إعدادات العرض
Hakika nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili miongoni mwa vidole vya Rahmaan (Mwingi wa rehema), kama moyo wa mtu mmoja, anaugeuza kokote atakako
Hakika nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili miongoni mwa vidole vya Rahmaan (Mwingi wa rehema), kama moyo wa mtu mmoja, anaugeuza kokote atakako
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Amri bin Aaswi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili miongoni mwa vidole vya Rahmaan (Mwingi wa rehema), kama moyo wa mtu mmoja, anaugeuza kokote atakako" Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu mwenye kuzigeuza nyoyo, zigeuze nyoyo zetu zielekee katika kukutii".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Kurdî Português සිංහල অসমীয়া Tiếng Việt ગુજરાતીالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili katika vidole vya Rahmaan kama moyo mmoja; anaugeuza kokote atakako; akitaka anausimamisha katika haki, na akitaka anaupotoa katika haki, na kuzigeuza kwake nyoyo zote ni kama kuugeuza moyo mmoja, hakuna jambo linaloweza kumshughulisha akaacha jambo jingine, kisha akaomba rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Mwenyezi Mungu mwenye kuzigeuza nyoyo, wakati mwingine katika utiifu na wakati mwingine katika maasi, na wakati mwingine katika kukutaja na wakati mwingine katika kughafilika, zigeuze nyoyo zetu zielekee katika utiifu wako.فوائد الحديث
Kumethibitishwa makadirio, nakuwa Mwenyezi Mungu anazielekeza nyoyo za waja wake kulingana na kadari aliyoziandikia juu yake.
Inampasa muislamu kudumu kumuomba Mola wake Mlezi kuthubutu katika haki na uongofu.
Kumhofu Mwenyezi Mungu na kufungamana nayeye peke yake asiye na mshirika.
Amesema Aajurri: Hakika watu wa haki humsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa sifa alizojisifu mwenyewe Aliyetakasika na kutukuka, na kwa sifa alizomsifu kwazo Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, na kwa zile walizomsifu kwazo Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na huu ndio msimamo wa wanachuoni katika wale waliofuata muongozo na wala hawakuzua. Mwisho. Watu wa sunna humthibitishia Mwenyezi Mungu aliyoyathibitisha yeye mwenyewe kwa nafsi yake katika majina na sifa pasina kupotoa, wala kukanusha wala kuhoji wala kufananisha, na wanamkanushia Mwenyezi Mungu yale aliyoyakanusha yeye mwenyewe juu nafsi yake, na wananyamaza katika yale ambayo mafundisho hayakueleza kuthibitisha au kukanusha, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakuna chochote mfano wake, naye ni Msikivu Mwenye kuona".
التصنيفات
Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.