إعدادات العرض
Kafara ya nadhiri ndio kafara ya kiapo
Kafara ya nadhiri ndio kafara ya kiapo
Imepokelewa kutoka kwa Uqba bin Aamir -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kafara ya nadhiri ndio kafara ya kiapo".
الترجمة
العربية Bosanski English فارسی Français Русский हिन्दी 中文 Bahasa Indonesia اردو Kurdî Português دری Македонски Tiếng Việt Magyar ქართული বাংলা ไทย অসমীয়া Hausa Nederlands ਪੰਜਾਬੀالشرح
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kafara ya kiapo cha jumla kisipoambatanishwa na kile anachokitaka au kukitaja: Ni kama kafara ya kiapo.فوائد الحديث
Nadhiri: Kisheria: Ni mtu anayelazimika kubeba sheria kujilazimisha yeye mwenyewe kwa hiari yake jambo fulani kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kafara ya kiapo: Ni kulisha masikini kumi au kuwavisha kama nguo, au kumuacha huru mtumwa kutoka katika utumwa, asipoweza basi ni kufunga siku tatu.
Hekima na sababu ya kuwekwa kafara ni Muislamu aiheshimu nadhiri, hivyo asiizoee, na isikae ulimini mwake.
Aina za nadhiri: 1- Nadhiri isiyoanishwa: Kama mtu kusema: "Nimetia nadhiri ikiwa nitapona" na akanyamaza akawa hakunuia nadhiri maalumu huyu atatakiwa kutoa kafara ya kiapo endapo atapona. 2- Nadhiri ya hamaki na ghadhabu: Nayo ni mtu kutundika nadhiri katika sharti, akiwa na lengo la kukataza jambo kutofanyika au kuwa msukumo wa jambo lifanyike, kama kusema: "Ikiwa nitakusemesha basi nifunge mwezi mzima", na hukumu yake: Apewe hiari kati kufanya alichojiwekea, au atoe kafara ya kiapo wakati atakapomsemesha. 3- Nadhiri ya halali: Mfano: "Natoa nadhiri kwa Mwenyezi Mungu kuwa nitavaa nguo yangu", na hukumu yake: Atapewa hiari kati ya kuvaa nguo au kutoa kafara ya kiapo. 4- Nadhiri ya machukizo: "Naweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kumpa talaka mke wangu", na hukumu yake: Ni sunna kwake kutoa kafara ya kiapo na asifanye alichotia nadhiri, na akikifanya hatolazimika kutoa kafara. 5- Nadhiri ya maasi: Mfano "Naweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ntakuja kuiba", na hukumu yake ni haramu kuitekeleza, na atatoa kafara ya kiapo, na akitekeleza atapata dhambi lakini hatolazimika kutoa kafara. 6- Nadhiri ya kumtii Mwenyezi Mungu: Mfano: "Naweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kuswali rakaa kadhaa" anakusudia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akiitundika katika sharti kama kupona kwa mgonjwa basi ni wajibu kutekeleza endapo sharti litapatikana, na asipoiambatanisha na chochote basi itakuwa wajibu kuitekeleza moja kwa moja.
التصنيفات
Viapo na Nadhiri.