إعدادات العرض
Nilikuwa nikimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitoa salamu kuliani kwake, na kushotoni kwake, mpaka ninaona weupe wa shavu lake
Nilikuwa nikimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitoa salamu kuliani kwake, na kushotoni kwake, mpaka ninaona weupe wa shavu lake
Kutoka kwa Sa'd radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa nikimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitoa salamu kuliani kwake, na kushotoni kwake, mpaka ninaona weupe wa shavu lake.
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية Português دری Македонски Magyar Tiếng Việt ქართული বাংলা Kurdî ไทย অসমীয়া Bahasa Indonesia Nederlands ਪੰਜਾਬੀالشرح
Ameeleza Sa'di bin Abii Waqasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba alikuwa akiona shavu la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na kugeuka kwake sana anapotoa salamu kwa ajili ya swala yake, kuliani kwake kwa ajili ya salamu ya kwanza, na kushotoni kwake kwa ajili ya salamu ya pili.فوائد الحديث
Sheria ya kupitiliza katika kugeuka katika upande wa kulia na upande wa kushoto.
Sheria ya kutoa salamu mbili kuliani na kushotoni.
Amesema Nawawi: Na lau mtu atatoa salamu mbili kuliani kwake au kushotoni kwake au mbele yake au ya kwanza kushotoni kwake na ya pili kuliani kwake swala yake itakuwa sahihi, lakini atakosa fadhila ya usahihi wake.
