إعدادات العرض
1- Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba, kwa paji la uso, na akaashiria kwa mkono wake katika pua yake, na mikono miwili na magoti mawili, na ncha za miguu miwili, na wala tusizikunje nguo na nywele
2- Yakuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Alikuwa akisema kati ya sijida mbili: Allaahumma ghfirlii, warhamnii, wa aafinii, wahdinii. warzuqnii (Ewe Mola wangu nisamehe, na unirehemu, na unipe afya, na uniongoze, na uniruzuku)
3- Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Alikuwa akinyanyua mikono yake usawa wa mabega yake anapofungua swala, na anapotoa takbira ya kurukuu, na anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu anainyanyua pia
4- Alinifundisha mimi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- tashahudi (tahiyatu), mkono wangu ukiwa katikati ya mikono yake kama anavyonifundisha sura katika Qur'ani
5- Linganeni sawa katika sijida, na asikunjue mmoja wenu mikono yake kama anavyokunjua mbwa
6- Enyi watu! Bila shaka nimefanya hivi ili muige na mjifunze swala yangu
7- Pindi mtakaposwali basi nyoosheni safu zenu, kisha akuongozeni mmoja wenu, atakapotoa takbira basi toeni takbira
8- Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi ndiye mtu niliyekaribu zaidi kwenu nyinyi swala yangu kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, bila shaka hii ndio ilikuwa swala yake mpaka alipoondoka duniani
9- Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni yule anayeiba swala yake" Akasema: Ataiba vipi swala yake? Akasema: "Hatimizi rukuu zake wala sijida zake
10- Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu anasema: "Sami'allaahu liman hamidah
11- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema kati ya sijida mbiliL "Rabbigh-firlii, Rabbigh-firlii
12- Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu