Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba

Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba, kwa paji la uso, na akaashiria kwa mkono wake katika pua yake, na mikono miwili na magoti mawili, na ncha za miguu miwili, na wala tusizikunje nguo na nywele".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu kamuamrisha wakati wa swala asujudu kwa viungo saba katika viungo vya mwili; navyo ni: Cha kwanza: Paji la uso: Nao ni ubapa wa uso ulioko juu ya pua na macho mawili, Na akaashiria -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa mkono wake katika pua yake, akieleza kuwa paji la uso na pua ni kiungo kimoja katika vile saba, na akitia msisitizo kwa mwenye kusujudu kuwa agusishe pua yake katika ardhi. Cha pili: na cha tatu: Ni mikono miwili. Cha nne na cha tano: Ni magoti mawili. Cha sita na cha saba: Ni vidole vya miguu miwili. Na akatuamrisha tusizifunge nywele zetu, au kuzikunja kunja nguo zetu katika ardhi wakati wa kusujudu kwa kuilinda ardhi (Isiguse paji la uso); bali tuziache mpaka zidondoke katika ardhi, ili zisujudu pamoja viungo.

فوائد الحديث

Uwajibu wa kusujudu katika swala juu ya viungo saba.

Karaha ya kukusanya nguo na nywele ndani ya swala.

Ni wajibu kwa mwenye kuswali atulizane ndani ya swala yake, na hii ni kwa kuweka viungo saba vya kusujudu juu ya ardhi, na atulizane hapo mpaka alete dua zote zilizopangwa na sheria.

Katazo la kufunga nywele hili ni maalumu kwa wanaume pasina wanawake; kwa sababu mwanamke ndani ya swala ameamrishwa kujisitiri

التصنيفات

Sifa za Swala.