إعدادات العرض
Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi ndiye mtu niliyekaribu zaidi kwenu nyinyi swala yangu kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, bila shaka hii ndio ilikuwa swala yake mpaka alipoondoka duniani
Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi ndiye mtu niliyekaribu zaidi kwenu nyinyi swala yangu kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, bila shaka hii ndio ilikuwa swala yake mpaka alipoondoka duniani
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Anasimulia yakuwa yeye alikuwa akitoa takbira katika swala zote za faradhi na zinginezo, ndani ya ramadhani na nje ya ramadhani, anatoa takbira anaposimama, kisha anatoa takbira wakati anarukuu, kisha anasema: Sami'allaahu liman hamidah, kisha anasema: Rabbanaa walakal hamdu, kabla hajasujudu, kisha anasema: 'Allaahu Akbaru' wakati anapoporomoka kwenda kusujudu, kisha anatoa takbira wakati ananyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, kisha anatoa takbira wakati anasujudu, kisha anatoa takbira wakati ananyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, kisha anatoa takbira wakati ananyanyuka kutoka katika kikao kwenda katika rakaa ya pili, na anafanya hivyo katika rakaa zote, mpaka anamaliza swala, kisha anasema anapomaliza swala: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi ndiye mtu niliyekaribu zaidi kwenu nyinyi swala yangu kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, bila shaka hii ndio ilikuwa swala yake mpaka alipoondoka duniani.
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча Lietuvių Kinyarwanda नेपाली తెలుగు Bosanski Italiano ಕನ್ನಡ Kurdî മലയാളം Oromoo Română Soomaali Shqip Српски Українська Wolof Moore Tagalog Malagasy தமிழ் Azərbaycan فارسی ქართული 中文 Magyarالشرح
Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- anapokea sehemu katika sifa ya swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na anaeleza kuwa alipokuwa akisimama katika sala anatoa takbira wakati ananyanyuka, nayo ni takbira ya kuhirimia swala, kisha anatoa takbira wakati anahama kwenda katika rukuu, na wakati anasujudu, na wakati anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, na wakati anasujudu sijida ya pili, na anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida hiyo, na anaponyanyuka katika rakaa mbili za mwanzo baada ya kikao cha tashahudi ya kwanza katika swala yenye rakaa tatu au nne, kisha anafanya hivyo katika swala nzima mpaka anamaliza, na alikuwa akisema anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu: Sami'allaahu liman hamidah, kisha anasema akiwa wima: Rabbanaa lakal hamdu. Kisha anasema Abuu Huraira wakati anapomaliza swala: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi swala yangu iko karibu zaidi kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- zaidi yenu, bali hii ndio ilikuwa sifa ya sala yake mpaka alipoondoka duniani.فوائد الحديث
Takbira inakuwa wakati wa kila kuinama na kunyanyuka isipokuwa wakati wa kunyanyuka kutoka katika rukuu, hapo atasema: Sami'allaahu liman hamidah.
Pupa ya Masahaba katika kumuiga Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kuhifadhi sunna yake.
التصنيفات
Sifa za Swala.