Pindi mtakaposwali basi nyoosheni safu zenu, kisha akuongozeni mmoja wenu, atakapotoa takbira basi toeni takbira

Pindi mtakaposwali basi nyoosheni safu zenu, kisha akuongozeni mmoja wenu, atakapotoa takbira basi toeni takbira

Kutoka kwa Hittwan bin Abdillah Ar-Raqashi amesema: Nilisali pamoja na Abuu Mussa Al-Ash'ariy swala moja, tulipofika katika kikao (cha tahiyatu) mtu mmoja akasema: Swala imefungamanishwa na wema na zaka, akasema: Abuu Mussa alipomaliza swala na akatoa salamu, akageuka na akasema: Ni nani kati yenu aliyesema neno kadhaa wa kadhaa? Akasema: Watu wote wakanyamaza, kisha akasema: Ni nani kati yenu aliyesema neno kadhaa wa kadhaa? Watu wote wakanyamaza, akasema: Huenda ukawa ni wewe uliyesema ewe Hittwan? Akasema: Hakika niliogopa utaninyamazisha kwa neno hilo, akasema mtu mmoja katika jamaa waliokuwepo: Mimi ndiye niliyesema, na sikukusudia kwa neno hilo ila kheri, Abuu Mussa akasema: Hivi hamjui ni vipi mtasema ndani ya swala zenu? hakika Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alituhutubia na akatubainishia sunna zetu na akatufundisha swala yetu, akasema: "Pindi mtakaposwali basi nyoosheni safu zenu, kisha akuongozeni mmoja wenu, atakapotoa takbira basi toeni takbira, na anaposema: "Ghairil maghdhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" [Suratul Fatiha: 7], basi semeni: Aaamiin (Ewe Mola wetu Mlezi tukubalie maombi) Atakujibuni Mwenyezi Mungu, atakapotoa takbira na akarukuu basi nanyi toeni takbira na mrukuu, kwani imamu anatakiwa kurukuu kabla yenu, na anyanyuke kabla yenu", akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:"Hiyo itakwenda na ile, na akisema: Samia'llaahu liman hamidah, semeni: Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, Mwenyezi Mungu anakusikieni, kwani Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- alisema kupitia ulimi wa Nabii wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi, na akitoa takbira akasujudu basi sujuduni, kwani imamu anatakiwa asujudu kabla yenu na anyanyuke kabla yenu", akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hiyo inakwenda ile, na akifika mahali pa kukaa basi kauli ya mwanzo ya mmoja wenu iwe ni: Attahiyyatut twayyibaatu as swalawaatu lillaah, assalaam alaika ayyuhan nabiyyu warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu alainaa wa alaa ibaadillaahis swaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu wa ash-hadu anna Muhammadan abduhu warasuuluhu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Swahaba Abuu Mussa Al-Ash'ary -Radhi za Allah ziwe juu yake- alisali swala moja, alipofika katika kikao cha tahiyatu ambacho kinatashahudi, mtu mmoja akasema miongoni mwa wasaliji walioko nyuma yake: Swala imeunganishwa ndani ya Qur'ani na wema na zaka, Abuu Mussa -Radhi za Allah ziwe juu yake- alipomaliza swala aliwageukia maamuma, akawauliza: Ni nani kati yenu aliyesema neno: Swala imeunganishwa ndani ya Qur'ani na wema na zaka?!, Watu wote wakanyamaza, na hakuzungumza yeyote kati yao, akarudia kuwauliza swali mara nyingine, alipoona hakuna alliyemjibu, Abuu Mussa -Radhi za Allah ziwe juu yake- akasema: Huenda ukawa ni wewe Hittwan ndiye uliyesema! Kwa ujasiri wake na ukaribu wake kwake, na mahusiano yake kwake, jambo ambalo haliwezi kupelekea kumtuhumu, na ili ampe msukumo msemaji wa uhakika kukiri, Hittwan akalikanusha hilo, na akasema, nilihofia unaweza kunikaripia kwa kudhani kuwa mimi ndiye niliyesema; na hapa sasa yule bwana akazungumza: Mimi ndiye niliyesema, na sikukusudia ila jambo la kheri, Abuu Mussa akasema kwa kumfundisha: Hivi hamjui ni nini mtasema ndani ya swala yenu?! Alisema hivi kwa kukemea kitendo hicho, kisha Abuu Mussa akaeleza kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwahutubia siku moja, akawabainishia sheria zao, na akawafundisha swala yao, akasema -Rehema na amani ziwe juu yake-: Mtakaposali basi nyoosheni safu zenu, na mlingane sawa, kisha mmoja miongoni mwao awasalishe watu, imamu atakapotoa takbira ya kuhirimia swala, basi toeni takbira mfano wake, na akisoma suratul Fatiha na akafikia: "Ghairil magh-dhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" [Fatiha: 7], Semeni: Aaamiin; mkifanya hivyo Mwenyezi Mungu atakujibuni maombi yenu, akitoa takbira na akarukuu basi toeni takbira na mrukuu; kwani imamu anarukuu kabla yenu na ananyanyuka kabla yenu msimtangulie; kwa sababu mahali alipowatangulia imamu ni katika kuwatangulia kurukuu, kutamalizika kwa kuchelewa kwenu kidogo baada ya yeye kunyanyuka kidogo, kitambo hicho kidogo kitapishana kidogo na kunyanyuka kwake, na hapo kiwango cha rukuu yenu kitakuwa sawa na rukuu yake, na imamu akisema: Samiallaahu liman hamidah, basi semeni: Allaahumma Rabbanaa walakal hamdu, waswaliji wakisema hivyo basi hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anasikia dua zao na kauli zao, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema kwa ulimi wa Nabii -Rehema na amani ziwe juu yake-:Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumuhimidi, kisha imamu akitoa takbira na kusujudu basi na maamuma wanatakiwa kutoa takbira na kusujudu, kwani imamu anatakiwa asujudu kabla yao, na anyanyuke kabla yao, kiwango hicho kidogo cha kusubiri kitakuwa sawa na kiwango chake, na hapo kiwango cha maamuma kitakuwa sawa na kiwango cha imamu, ana akifika katika kikao cha tahiyatu, na iwe kauli ya mwanzo ya mwenye kusali ni: "Attahiyyatut twayyibaatu asswalawaatu lillaah" Ufalme na kubakia na utukufu wote unamstahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, na vile vile swala tano zote ni za Mwenyezi Mungu, "Assalaamu alaika ayyuhan nabiyyu warahmatullaahi wabarakaatuh", "Assalaamu alainaa walaa ibaadillaahis swaalihiin, muombe Mwenyezi Mungu akusalimishe na kila aibu na maafa, na mapungufu na maovu; na tunamtaja Muhammadi pekee kwa kumtakia amani, kisha tunajitakia amani wenyewe, kisha tunawatakia amani waja wema wa Mwenyezi Mungu wale wenye kutekeleza haki zilizo juu yao za Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za waja wake, kisha tunashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na tunashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na Mtume wake.

فوائد الحديث

kumebainishwa namna miongoni mwa aina za tashahudi.

Maneno ya swala na vitendo vyake lazima yawe yamethibiti kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, haruhusiwi yeyote kuzua ndani ya swala kuli au kitendo ambacho hakikuthibiti ndani ya sunna.

Haitakiwi kumtangulia imamu au kuchelewa kumfuata, na sheria kwa maamuma ni kumfuata imamu katika vitendo vyake.

Kumetajwa yale aliyokuwa akiyafanya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ikiwemo kutilia umuhimu kufikisha ujumbe, na kuufundisha umma wake hukumu za dini.

Imamu ndio kiigizo kwa maamuma, hatakiwi kumtangulia katika matendo ya swala na wala asiende nae sawa, na wala asichelewe kumfuata, bali kumfuata kwake kuanzie baada ya kuhakikisha kuwa kaingia katika kitendo anachotaka kukifanya, na sunna ni kumfuata.

Sheria ya kunyoosha safu katika swala.

التصنيفات

Sifa za Swala., Hukumu ya Imamu na Maamuma.