إعدادات العرض
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu anasema: "Sami'allaahu liman hamidah
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu anasema: "Sami'allaahu liman hamidah
Imepokewa kutoka kwa Abuu Aufaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu anasema: "Sami'allaahu liman hamidah, Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati wamil al Ardhwi wamil amaashi ita min shai in ba'ad".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча Lietuvių Kinyarwanda नेपाली తెలుగు Bosanski ಕನ್ನಡ Kurdî മലയാളം Oromoo Română Italiano Soomaali Shqip Српски Українська Wolof Moore Português Tagalog Malagasy தமிழ் Azərbaycan فارسی ქართული 中文 Magyarالشرح
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuuu ndani ya swala, anasema: " Sami'allaahu liman hamidah", Yaani: Atakayemhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamjibu, na atakubali himidi zake na atamlipa, kisha atamhimidi kwa kusema: Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati, wamil al Adhwi wamil amaa shi ita min shai in baad", himdi zenye kujaza mbingu na ardhi na vilivyo kati yake, na zinajaza ayatakayo Mwenyezi Mungu.فوائد الحديث
Kumebainishwa anayotakiwa kusema mwenye kusali anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu.
Sheria ya kulingana sawa na utulivu baada ya kuinuka kutoka katika rukuu; kwa sababu haiwezekani aseme dhikiri hii ila baada ya kusimama wima na kutulia.
Dhikiri hii ni sheria katika swala zote, sawa sawa ziwe za faradhi au za sunna.