إعدادات العرض
Alinifundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake, namna ya tashahudi iletwayo ndani ya sala, na kiganja changu kikiwa kati ya viganja vyake, kama anavyonifundisha sura ndani ya Qur'ani
Alinifundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake, namna ya tashahudi iletwayo ndani ya sala, na kiganja changu kikiwa kati ya viganja vyake, kama anavyonifundisha sura ndani ya Qur'ani
Kutoka kwa bin Masoud radhi za Allahi ziwe juu yake amesema: Alinifundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake, namna ya tashahudi iletwayo ndani ya sala, na kiganja changu kikiwa kati ya viganja vyake, kama anavyonifundisha sura ndani ya Qur'ani: "Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu" Tafsiri yake: Maamkizi (Amani) ni ya Mwenyezi Mungu, na swala na vile vilivyo vizuri, amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, nashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni mjumbe wake. Na katika lafudhi yao nyingine: "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Amani, atakapokaa mmoja wenu katika swala basi na aseme: Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, akisema hivyo, basi dua hii itampata kila mja mwema wa Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu, kisha baada ya hapo atachagua maombi yoyote anayotaka kuomba".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी සිංහල ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Tiếng Việt ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or नेपाली Malagasy Kinyarwanda Română తెలుగు Lietuvių Oromoo മലയാളം Nederlands Soomaali Shqip Српски Українська Deutsch ಕನ್ನಡ Mooreالشرح
Mtume Rehema na amani ziwe juu yake alimfundisha bin Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake tashahudi inayosemwa ndani ya swala, akiwa kaweka mkono wake ndani ya mikono yake, ili asogeze karibu umakini wa bin Masoud. Na alifanya hivyo kama anavyomfundisha sura ndani ya Qur'ani jambo linaloonyesha kuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake aliitilia umuhimu tashahudi kwa matamshi na maana yake pia. Akasema: "Attahiyyaatu lillaah" (Maamkizi Mema ni ya Mwenyezi Mungu): Nayo ni kila kauli au kitendo kinachojulisha kutukuza, vyote hivyo vinastahiki kufanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Swala": Nazo ni swala zinazofahamika za Faradhi na za sunna zote hizo ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Mambo mazuri": Nayo ni maneno na matendo na sifa njema zinazojulisha ukamilifu, zote hizo zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Amani iwe kwako ewe Nabii na Rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake": Hii ni dua yake ya kuomba amani na uzima dhidi ya kila maafa na yenye kuchukiza, na kuomba ziada na wingi kutoka katika kila kheri. "Amani iwe juu yetu na kwa waja wema wa Mwenyezi Mungu": Hii ni dua ya kuomba uzima kwa kila mwenye kuswali na kwa kila mja mwema aliye mbinguni na ardhini. "Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu": Yaani ninakiri kukiri kwenye kuondoa shaka kabisa yakuwa hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. "Na kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake": Ninakiri kwake kuwa ni mja na kapewa ujumbe wa mwisho. Kisha akamhimiza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuswali achague katika dua aitakayo.فوائد الحديث
Mahala pa tashahudi hii ni wakati wa kukaa baada ya sijida ya mwisho katika kila swala, na baada ya rakaa ya pili katika swala za rakaa tatu na nne.
Uwajibu wa tashahudi katika swala, na inafaa akatoa tashahudi kwa lafudhi yoyote katika lafudhi za tashahudi katika zile zilizothibiti kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake.
Inafaa kuomba dua ndani ya swala kwa jambo alitakalo mtu madam si dhambi.
Inapendeza kuanza kujiombea mwenyewe kwanza katika dua.
التصنيفات
Sifa za Swala.