إعدادات العرض
Enyi watu! Bila shaka nimefanya hivi ili muige na mjifunze swala yangu
Enyi watu! Bila shaka nimefanya hivi ili muige na mjifunze swala yangu
Kutoka kwa Abuu Hazim bin Dinari: Anasimulia kuwa watu fulani walikuja kwa Sahli bin Sa'di As-saaidi, wakiwa wamepatwa na shaka kuhusu mimbari (ya Mtume) ilitengenezwa kwa mti gani, wakamuuliza kuhusu hilo, akasema: Wallahi mimi ninajua imetokana na mti gani, na niliiona tangu siku ya kwanza ilipowekwa, na siku ya kwanza kuikalia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, aliagiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa fulani -Mwanamke aliyekuwa mke wa mmoja kati ya Maanswari (Watu wa Madina) -Sahli alimtaja kwa jina lake-: "Muamrishe kijana wako seremala anitengenezee kibao niwe nakalia ninapo zungumza na watu", akamuamrisha akatengeneza kutokana na mti wa Twarfa (Mti mfano wa mkaratusi) hupatikani msituni, kisha akaileta, yule mama akaiagiza kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akaamrisha ikawekwa hapa, kisha nikamuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa juu yake na akatoa takbira (Allahu Akbaru) akiwa juu yake, kisha akarukuu akiwa ju yake, kisha akashuka kinyumenyume akasujudu mwishoni mwa mimbari, kisha akarudi, alipomaliza swala yake akawageukia watu kisha akasema: "Enyi watu! Bila shaka nimefanya hivi ili muige na mjifunze swala yangu".
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча Lietuvių Kinyarwanda नेपाली മലയാളം తెలుగు Bosanski Italiano ಕನ್ನಡ Kurdî Oromoo Română Soomaali Shqip Српски Українська Wolof Moore Tagalog O‘zbek Malagasy தமிழ் Azərbaycan فارسی ქართული 中文 Magyarالشرح
Walikuja baadhi ya watu kwa mmoja kati ya Masahaba wakimuuliza kuhusu Mimbari ya Mtume aliyoitumia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ilitengenezwa kwa kitu gani? Na walikuwa wamekwisha bishana na kuzozana katika hilo, akawaeleza kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-aliagiza kwa mwanamke wa ki Answari alikuwa na mtumishi seremala, akamwambia: Mwamrishe kijana wako anitengenezee Mimbari nikalie wakati nikizungumza na watu, mama yule akakubali ombi hilo, na akamuamrisha kijana wake amtengeneze Mimbari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokana na mti wa Twarfaa (Mti mfano wa mkaratusi), kijana alipomaliza kazi, yule mama aliaigiza kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mtume akaamrisha iwekwe mahala pake msikitini, kisha akaswali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa juu yake, na akatoa takbira akiwa juu yake, kisha akarukuu akiwa juu yake, kisha akashuka akiwa anatembea kwa nyuma bila ya kugeuka kutazama nyuma, akasujudu mwishoni mwa Mimbari, kisha akarudi, alipomaliza swala akawageukia watu, na akasema: Enyi watu!, Bila shaka nimefanya hivi ili muige na mjifunze swala yangu.فوائد الحديث
Sunna ya kuweka Mimbari na muhutubu kupanda juu yake, na faida yake ni kufikisha sauti mbali.
Kufaa kusali juu ya Mimbari kwa ajili ya kufundisha, na inafaa kwa imamu kuwa juu kuliko maamuma kukiwa na haja.
Inafaa kuwaomba msaada watu wenye ufundi fulani katika haja za waislamu.
Inafaa kufanya harakati ndogo ndani ya swala kukiwa na haja.
Inafaa maamuma kumtazama imamu wake akiwa ndani ya swala; ili ajifunze kutoka kwake, nakuwa hilo haliondoi utulivu.
التصنيفات
Sifa za Swala.