إعدادات العرض
Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni yule anayeiba swala yake" Akasema: Ataiba vipi swala yake? Akasema: "Hatimizi rukuu zake wala sijida zake
Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni yule anayeiba swala yake" Akasema: Ataiba vipi swala yake? Akasema: "Hatimizi rukuu zake wala sijida zake
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni yule anayeiba swala yake" Akasema: Ataiba vipi swala yake? Akasema: "Hatimizi rukuu zake wala sijida zake".
[Sahihi] [Imepokelewa na Ibnu Hibaan]
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча Lietuvių Kinyarwanda नेपाली తెలుగు Bosanski Italiano ಕನ್ನಡ Kurdî മലയാളം Oromoo Română Soomaali Shqip Српски Українська Wolof Tagalog Moore Malagasy தமிழ் Azərbaycan فارسی ქართული 中文 Magyarالشرح
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwizi mbaya zaidi kuliko wote ni yule anayeiba swala yake; na hii ni kwakuwa; kuchukua mali ya mtu mwingine huenda mtu akanufaika nayo duniani, tofauti na mwizi huyu, kwa sababu kaiba haki ya nafsi yake katika thawabu na malipo, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na vipi mtu anawezaiba kutoka katika swala yake? Akasema: Kwa kutotimiza rukuu zake wala sijida zake; na hii ni pale anapofanya haraka kutoka katika rukuu na sijida, hazileti katika namna ya ukamilifu.فوائد الحديث
Umuhimu wa kuifanya vizuri sala, na kuzileta nguzo zake taratibu na kwa utulivu.
Amemsifu mtu asiyetimiza rukuu yake na sijida yake kuwa ni mwizi, ikiwa ni ishara ya kulichukia hilo, na tahadhari juu ya uharamu wake.
Uwajibu wa kutimiza rukuu na sijida ndani ya swala na kutulizana ndani yake.