إعدادات العرض
Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu
Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu
Kutoka kwa Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika shetani amekaa kati yangu na swala yangu na kisomo changu ananichanganya, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu", anasema: Nikafanya hivyo Mwenyezi Mungu akamuondosha kwangu.
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча Lietuvių Kinyarwanda नेपाली తెలుగు Bosanski ಕನ್ನಡ Kurdî മലയാളം Oromoo Română Italiano Soomaali Shqip Српски Українська Wolof Moore Tagalog Malagasy தமிழ் Azərbaycan فارسی ქართული 中文 Magyarالشرح
Alikuja Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake- kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika Shetani ameziba kati yangu na swala yangu, na amenizuilia na kupata utulivu ndani yake, na amenichanganyia kisomo changu na amenitia wasi wasi ndani yake, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Huyo ni Shetani aitwaye Khinzab, ukihisi hali hii basi taka kinga kwa Allah, na utake ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme mate kushotoni kwako mara tatu, Othman anasema: Nikafanya aliyoniamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mwenyezi Mungu akaniondolea hali hiyo.فوائد الحديث
Umuhimu wa utulivu na kuhudhurisha moyo ndani ya sala, na kuwa Shetani anajitahidi kutia tashiwishi na shaka ndani yake.
Sunna ya kutaka ulinzi kutokana na shetani wakati wa wasi wasi wake ndani ya sala, pamoja na kutema kushoto mara tatu.
Kumebainishwa waliyokuwa nayo Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- katika swala la kurudi kwao kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika yale yanayojitokeza kwao miongoni mwa changamoto ili azitatue.
Maisha ya nyoyo za Masahaba, na kwamba hima yao kubwa ilikuwa ni Akhera.