إعدادات العرض
1- Ametenda dhambi mja, akasema: Ewe Mola wangu nisamehe mimi dhambi langu, akasema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: Mja wangu katenda dhambi, na akajua kuwa ana Mola anayesamehe dhambi, na analichukua dhambi
2- Atakayesema: Sub-haana llaahi wabihamdihi- Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake- kwa siku mara mia moja, atasamehewa makosa yake hata kama yatakuwa mfano wa povu la bahari
3- Atakayesema: Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul Mulku walahul Hamdu, Wahuwa a'laa kulli shay in Qadiir (Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika, Ufalme ni wake, na sifa njema ni zake, Naye juu ya kila kitu ni muweza), akasema hivyo mara kumi, Atakuwa sawa na aliyeacha huru nafsi nne katika watoto wa Ismail.
4- Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema mmoja wenu: Allahu Akbaru Allahu Akbaru
5- Alitoka Muawiya- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akakuta duara msikitini, akasema: Nini kimewakalisheni? wakasema: tumekaa tunamtaja Mwenyezi Mungu
6- Je nikujulisheni matendo yenu bora, na matukufu mbele ya mfalme wenu
7- Wametangulia watu wa kipekee
8- Nilikutana na Ibrahimu usiku niliochukuliwa, Akasema: Ewe Muhammadi wafikishie umma wako salamu zangu, na uwaeleze kuwa pepo ina udongo mzuri, ina maji matam, nakuwa imenyooka na kulingana sawa, nakuwa mimea yake: ni (kusema) Sub-haana llaah -Ametakasika Mwenyezi Mungu, Na Alhamdulillaah -Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, Na Laa ilaaha illa llaah -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Allaahu Akbar -Mwenyezi Mungu Mkubwa.
9- Hakuna watu wowote watasimama katika kikao ambacho hawamtaji Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, isipokuwa watanyanyuka mithili ya mzoga wa punda, na wanakua na majuto
10- Mtakapo msikia muadhini basi semeni mfano wa yale anayo yasema, kisha mnitakie rehema
11- Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu