Hivi kwani hajakuwekeeni Mwenyezi Mungu mambo mnayoweza kutoa sadaka: Hakika katika kila tasbihi (kauli ya sub-haanallaah) ni sadaka, na kila takbira (Allahu Akbaru) ni sadaka, na kila tahmidi (Alhamdulillah) ni sadaka, na kila tahalili (Laa ilaaha illallaahu) ni sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka,…

Hivi kwani hajakuwekeeni Mwenyezi Mungu mambo mnayoweza kutoa sadaka: Hakika katika kila tasbihi (kauli ya sub-haanallaah) ni sadaka, na kila takbira (Allahu Akbaru) ni sadaka, na kila tahmidi (Alhamdulillah) ni sadaka, na kila tahalili (Laa ilaaha illallaahu) ni sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka, na katika kiungo cha siri cha mmoja wenu kuna sadaka

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba watu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake walisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamechukua malipo mengi wenye utajiri: Wanaswali kama tunavyoswali na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka katika mali yao ya akiba. Akasema: Hivi kwani hajakuwekeeni Mwenyezi Mungu mambo mnayoweza kutoa sadaka: Hakika katika kila tasbihi (kauli ya sub-haanallaah) ni sadaka, na kila takbira (Allahu Akbaru) ni sadaka, na kila tahmidi (Alhamdulillah) ni sadaka, na kila tahalili (Laa ilaaha illallaahu) ni sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka, na katika kiungo cha siri cha mmoja wenu kuna sadaka" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi yawezekanaje akidhi mmoja wetu matamanio yake kisha awe na malipo? Akasema: Mnasemaje ikiwa atakiweka katika haramu, je atakuwa na mzigo wa dhambi? basi ndivyo hivyo akikiweka katika halali atakuwa na malipo".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Walilalamikia baadhi ya mafukara wa kiswahaba hali ya umasikini wao kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kutotoa kwao sadaka kwa mali ili wapate malipo mengi kama walivyoyapata ndugu zao wenye mali nyingi na ili na wao wafanye kheri kama wao; kiasi ambacho wao wanaswali kama tunavyoswali, na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka kwa mali yao ya ziada na sisi hatutoi! Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaelekeza katika yale wanayoyaweza katika sadaka, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwani hakukujaalieni Mwenyezi Mungu vile mnavyoweza kuvitoa sadaka kwa ajili nafsi zenu?! Kwani kauli yenu: "Sub-haanallaah" Inakuwa kwenu na malipo ya sadaka, na vile vile kauli: "Allaahu Akbar" ni sadaka, na kauli: "Alhamdulillaah" ni sadaka, na kauli: Laa ilaaha illa llaah" ni sadaka, na kuamrisha mema" ni sadaka, na "kukataza maovu" ni sadaka, bali hata katika tendo la ndoa la mmoja wenu kwa mke wake ni sadaka. Wakashangaa, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi akidhi mmoja wenu matamanio yake na awe na malipo katika hilo?! Akasema: Hivi mwaonaje kama akiweka katika haramu kama zinaa au kinginecho, je, atakuwa na madhambi? Hivyo hivyo akiweka katika halali anakuwa na malipo.

فوائد الحديث

Kushindana kwa Maswahaba katika kufanya kheri, na pupa yao ya kupata malipo na fadhila kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kukithiri kwa njia za amali za kheri, nakuwa zinakusanya kila amali anayoifanya muislamu kwa nia njema na lengo zuri.

Urahisi wa Uislamu na wepesi wake, kila muislamu anapata anayoweza kuyafanya ili amtii Mwenyezi Mungu kwayo.

Amesema Nawawi: Na katika hili kuna dalili yakuwa mambo ya halali yanaweza kuwa ibada kwa nia ya kweli, tendo la ndoa linakuwa ibada atakaponuia kukidhi haki ya mke na kushiriki naye kwa wema ambao ameamrishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kutafuta mtoto mwema, na kuilinda nafsi yake na nafsi ya mke wake na kujizuia wote wawili na kutazama haramu, au kuifikiria, au kutamani kufanya, au mengineyo katika malengo mazuri.

Amepiga mfano na kupima kwa akili; ili jambo liwe wazi na liingie vizuri ndani ya nafsi ya msikilizaji.

التصنيفات

Sadaqa za kujitolea., Fadhila za Adh-kaar.