إعدادات العرض
1- Haijawahi kupunguza sadaka chochote katika mali, Na hajawahi kumzidishia Mwenyezi Mungu mja kwa usamehevu (wake) ispokuwa utukufu, na hajawahi kunyenyekea yeyote ispokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimnyanyua
2- Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu utapewa
3- Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa kuna Malaika wawili wanateremka,anasema mmoja wao: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mtoaji badala,na anasema mwingine:Ewe Mwenyezi Mungu mpe mzuiaji hasara
4- Matendo yapo ya aina sita na watu wapo wako aina nne, basi kuna watu wa aina mbili wanaostahiki malipo, na malipo yao huwa sawa na matendo yao, na jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na jema moja huzidishwa mpaka kufikia mema mia saba