Hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ataongeleshwa na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama bila ya kuwapo na mkalimani yeyote kati yake na Yeye (Allah)

Hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ataongeleshwa na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama bila ya kuwapo na mkalimani yeyote kati yake na Yeye (Allah)

Kutoka kwa Ka'bu bin Hatim -radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ataongeleshwa na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama bila ya kuwapo na mkalimani yeyote kati yake na Yeye (Allah). Atatazama kuliani kwake, na wala hataona kitu chochote isipokuwa matendo yake aliyotanguliza. Kisha ataangalia kushotoni kwake, na wala hataona kitu chochote isipokuwa matendo yake aliyotanguliza. Na ataangalia mbele yake, na hataona isipokuwa Moto mbele ya uso wake. Basi uepukeni Moto hata kama ni kwa nusu ya tende."

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alieleza Mtume rehema amani ziwe juu yake kuwa kila Muumini atasimama mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama peke yake, na kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atazungumza naye bila ya muwakilishi, na hakuna mkalimani baina yao wa kutafsiri maneno, hivyo atatazama kulia na kushoto kutokana na hofu kali, labda atapata njia ya kwenda ili aweze kuokolewa na moto uliombele yake. Akitazama upande ulioko kuliani kwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza katika matendo mema, na akitazama kushotoni kwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza katika matendo mabaya, na akitazama mbele yake hatoona isipokuwa moto, na hatoweza kuukwepa, kwani hakuna budi ni lazima apite juu daraja (Swirat). Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Wekeni kinga kati yenu na moto, kama kutoa sadaka na matendo mema, walau kwa kitu kidogo kama nusu ya tende.

فوائد الحديث

Himizo la kutoa sadaka hata kama itakuwa ndogo, na kujipamba na mambo mazuri, na kuamiliana kwa upole na maneno laini.

Ukaribu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake siku ya Kiyama, kiasi kwamba hapatokuwa na kizuizi kati yao, wala muwakilishi wala mkalimani, basi muumini achukue tahadhari asijekwenda kinyume na amri za Mola wake Mlezi.

Ni lazima kwa mtu asidharau anachokitoa sadaka, hata kama ni kidogo, kwani ni kinga ya kutoingia motoni.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake., Sadaqa za kujitolea.