إعدادات العرض
Matendo yapo ya aina sita na watu wapo wako aina nne, basi kuna watu wa aina mbili wanaostahiki malipo, na malipo yao huwa sawa na matendo yao, na jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na jema moja huzidishwa mpaka kufikia mema mia saba
Matendo yapo ya aina sita na watu wapo wako aina nne, basi kuna watu wa aina mbili wanaostahiki malipo, na malipo yao huwa sawa na matendo yao, na jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na jema moja huzidishwa mpaka kufikia mema mia saba
Imepokelewa kutoka kwa Khuraimu Bin Faatik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Matendo yapo ya aina sita na watu wapo wako aina nne, basi kuna watu wa aina mbili wanaostahiki malipo, na malipo yao huwa sawa na matendo yao, na jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na jema moja huzidishwa mpaka kufikia mema mia saba, Basi wawili wenye kustahiki malipo ni: Yeyote atakaye kufa hali yakuwa hajamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia Peponi, na atakaye kufa hali ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote basi ataingia Motoni, na ama yule ambaye atalipwa kwa namna alivyokusudia ni yeyote atakaye kusudia kufanya jambo jema mpaka moyo wake ukahisi kuwa umetenda na Mwenyezi Mungu akajua kutenda kwake huko basi mtu huyo ataandikiwa jema moja, na atakaye fanya kosa ataandikiwa kosa moja, na atakaye fanya jema moja basi hulipwa kwa kumi mfano wake, na mwenye kutoa chochote katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi atalipwa kwa kila kimoja kwa mara mia saba, ama watu walivyogawanyika kuna miongoni mwao waliokunjuliwa mambo yao hapa Duniani na wakawa na maisha duni huko Akhera, na kuna wenye maisha Duni hapa duniani na wakakunjuliwa maisha yao huko Akhera, na kuna wenye maisha duni hapa duniani na pia Akhera, na wakakunjuliwa maisha yao hapa duniani na kesho Akhera."
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Español Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe Bosanski සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa മലയാളം తెలుగు ไทย پښتو অসমীয়া Shqip دری Ελληνικά Български Fulfulde Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy or Română Kinyarwanda Српски тоҷикӣ O‘zbek नेपाली Moore Kurdî Oromoo Wolof Français Tagalog Azərbaycan Українська bm தமிழ் ქართული Deutsch Português Македонски Magyar فارسی Lingala Русский 中文الشرح
Alieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yapo aina sita, na watu wamegawanyika katika makundi manne, nayo ni: Kundi la kwanza: Yeyote atakaye kufa na hakumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote anastahiki kuingia peponi. Kundi la pili: Yeyote atakaye kufa hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu kingine anastahiki kuingia motoni na atakaa humo milele. Na matendo hayo mawili ndiyo haki mbili za msingi. Kundi la tatu: Kukusudia kufanya wema, basi yeyote atakaye kusudia kufanya jema na akawa mkweli katika makusudio yake mpaka akahisi kweye moyo wake kuwa hili ndilo kusudio langu, kisha likamtokea jambo la kumzuia asifanye alichokikusudia katika wema huu, basi huandikiwa thawabu za wema kamili. Kundi la nne: Kufanya tendo baya; Yeyote atakaye fanya tendo baya basi huandikiwa kosa moja. Na matendo hayo mawili: Ndiyo hulipwa sawa sawa bila ya kuzidisha. Kundi la Tano: Jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na malipo hayo ni kwa mwenye kukusudia kufanya wema na akaufanya wema huo, basi huandikiwa mema kumi. kundi la sita: Jema moja hulipwa sawa na mema mia saba, na malipo hayo ni kwa mwenye kutoa kitu kimoja katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hulipwa kwa kitu hiki kimoja kwa mema mia saba, na haya ni kutokana na fadhila za Mwenyezi Mungu aliyetakasika na Kutukuka, na ukarimu wake kwa waja wake. Ama aina Nne ya watu ni hawa: Aina ya kwanza: Ni mtu ambaye amekunjuliwa mambo yake hapa Duniani kwa upande wa riziki, ananeemeka humo na hupata akitakacho, lakini ni mwenye dhiki na tabu kubwa Akhera na mwisho wake ni kuingia motoni, na huyo ni tajiri wa kikafiri. Aina ya pili: Ni mtu mwenye dhiki hapa Duniani upande wa riziki, lakini amekunjuliwa huko Akhera, na mwisho wake ni kuingia Motoni, na huyo ni muumini fakiri. Aina ya tatu: Ni mtu mwenye dhiki hapa Duniani na Akhera, naye ni kafiri fukara. Aina ya nne: Ni mtu aliyekunjuliwa mambo yake hapa Duniani na Akhera, naye ni muumini tajiri.فوائد الحديث
Ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu kwa waja wake na kuwazidishia mambo mema.
Uadilifu wa Mwenyezi Mungu na ukarimu wake, pale alipo amiliana nasi kwenye makosa kwa uadilifu, hivyo basi akafanya malipo ya kosa moja ni moja hivyo hivyo.
Ukubwa wa dhambi ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu, katika hilo kunapelekea kuharamishiwa kuingia peponi.
Kumewekwa wazi utukufu na ubora wa kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Ongozeko la thawabu za kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, linaanzia ziada ya mia saba; Kwa sababu kutoa kunasaidia kuliinua neno la Mwenyezi Mungu.
Kumewekwa wazi aina za watu na tofauti zao.
Mwenyezi Mungu humkunjulia muumini na asiyekuwa mumini hapa Duniani, na wala hamkunjulii Akhera isipokuwa muumini tu.