إعدادات العرض
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mimi nikupe
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mimi nikupe
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mimi nikupe".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు မြန်မာ ไทย Deutsch 日本語 پښتو অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands ئۇيغۇرچە தமிழ் دری Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy Română Kinyarwanda नेपाली Српски Soomaali Moore Українська Български Wolof Azərbaycan ქართული тоҷикӣ bmالشرح
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Toa ewe mwanadamu -katika matumizi ya wajibu na ya hiyari- nikukunjulie na nikupe badala ya hicho na nikubariki ndani yake.فوائد الحديث
Himizo la kutoa sadaka na kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Kutoa katika njia za heri ni miongoni mwa sababu kubwa za kupata baraka katika riziki na kuzidishwa kwake, na Mwenyezi Mungu kumpa badala mja katika kile alichokitoa.
Hadithi hii ni katika zile anazozipokea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithil Qudsi au Hadithil Ilahi, nayo ni ile ambayo tamko lake na maana yake inatoka kwa Allah, isipokuwa haina upekee kama wa Qur'ani inaojipambanua nayo kwa vingine, ikiwa kisomo chake kutumika katika ibada, na kuwa twahara kabla ya kusoma, na kuwashinda watu kwa changamoto zake, na mengineyo.