Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama Sa'di amefariki, ni sadaka ipi bora ya kumfanyia? Akasema: "Maji" Akasema: tukachimba kisima, na akasema: Kisima hiki ni kwa ajili ya mama Sa'di

Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama Sa'di amefariki, ni sadaka ipi bora ya kumfanyia? Akasema: "Maji" Akasema: tukachimba kisima, na akasema: Kisima hiki ni kwa ajili ya mama Sa'di

Kutoka kwa Sa'di bin Ubada radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakwamba amesema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama Sa'di amefariki, ni sadaka ipi bora ya kumfanyia? Akasema: "Maji" Akasema: tukachimba kisima, na akasema: Kisima hiki ni kwa ajili ya mama Sa'di.

الشرح

Alifariki mama Sa'di bin Ubada radhi za Allah ziwe juu yake, akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni aina ipi bora ya sadaka ili aitoe kwa niaba ya mama yake? Akamueleza rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa sadaka bora ni maji, akachimba kisima na akakifanya kuwa sadaka kwa ajili ya mama yake.

فوائد الحديث

Kumeelezwa kuwa maji ndio sadaka bora zaidi.

Alimuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Sa'di katika sadaka ya maji; kwa sababu ndio inamanufaa mapana katika mambo ya dini na dunia, na kwa sababu ya joto kali na haja ya watu na uchache wa maji.

Hii ni dalili kuwa malipo ya sadaka yanawafikia maiti.

Wema wa Sa'di bin Ubada kwa mama yake radhi za Allah ziwe juu yao.

التصنيفات

Waq'fu., Sadaqa za kujitolea.