إعدادات العرض
Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini
Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema huku akiwa juu ya Mimbari, na akataja sadaka, na kujizuia kuomba, na kuombaomba: "Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini, mkono wa juu: Ni ule unaotoa, na mkono wa chini: Ni ule unaoomba".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî தமிழ் Magyar ქართული Română অসমীয়াالشرح
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitaja sadaka, na kujizuia kuombaomba, aliyasema hayo wakati akihutubia katika Mimbari; kisha akasema: Mkono wa juu wenye kutoa sadaka ni bora na unapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko mkono wa chini wenye kuomba.فوائد الحديث
Hapa kuna fadhila za ukarimu na utoaji katika njia za kheri, na ubaya wa kuombaomba.
Hapa kuna himizo la kujizuia kuomba, na kuwaepuka watu, na himizo la kufanya mambo matukufu, na kuacha yenye udhalili, na Mwenyezi Mungu anapenda mambo ya juu zaidi.
Mikono ina aina nne katika ubora, kama ifuatavyo: Wa juu zaidi ni ule unaotoa, kisha unaojizuia kuchukua, kisha unaopokea pasina kuomba, kisha unafuata wa chini kuliko hiyo, ule unaoomba.