Mja alifanya dhambi akasema: Ee Mola wangu nisamehe dhambi yangu

Mja alifanya dhambi akasema: Ee Mola wangu nisamehe dhambi yangu

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, katika yale anayoyasimulia kutoka kwa Mola wake Mtukufu, amesema: "Mja alifanya dhambi akasema: Ee Mola wangu nisamehe dhambi yangu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, na humsitiri kwa ndambi hiyo au humuadhibu kwa kutenda dhambi, kisha akarudi tena akatenda dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi yangu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, na ana adhibu kwa kutenda dhambi, fanya utakavyo nimekusamehe".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anasimulia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mola wake Mlezi ya kwamba mja anapofanya dhambi kisha akasema: Ewe Mola wangu nisamehe dhambi yangu, Mwenyezi Mungu husema: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, akamsitiri na akamsamehe, au akamuadhibu, basi hakika nimemsamehe. Kisha mja akarudi akafanya dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi yangu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, akamsitiri na akamsamehe, au akamuadhibu, basi kwa hilo nimemsamehe mja wangu. Kisha mja akarudi akafanya dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi langu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, akamsitiri na akamsamehe, au akamuadhibu, basi kwa hilo nimemsamehe mja wangu, afanye atakavyo madamu kila anapofanya dhambi analiacha na anajuta na anaazimia kutolirudia dhambi hilo mara nyingine, madamu ataendelea kufanya hivi, anatenda dhambi na anatubia nitaendelea kumsamehe, kwani toba hubomoa yaliyo kabla yake.

فوائد الحديث

Upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake na kuwa mwanadamu vyovyote vile atakavyotenda dhambi, vyovyote vile atakavyofanya, atakapotubia kwake na akarejea basi Mwenyezi Mungu humsamehe.

Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu hutumai kupata msamaha wa Mola wake Mlezi, na huogopa adhabu yake, hivyo huenda mbio kutubia na wala haendelei kubaki katika maasi.

Sharti za toba sahihi: Ni kujiondoa katika dhambi, na kulijutia, na kutia nia ya kutolirudia dhambi, na toba ikiwa ni katika mali za watu au heshima zao au nafsi, hapo huongezeka sharti la nne, nalo: Ni kujivua kutoka kwa mwenye haki yake, au kumpa haki yake.

Umuhimu wa elimu ya kumjuwa Mwenyezi Mungu elimu ambayo humfanya mja kujua mambo ya dini yake, akatubia kila anapokosea, hakati tamaa wala hafanyi jeuri kwa kuendelea kubaki katika dhambi.

التصنيفات

Fadhila za Adh-kaar.