Hakuna watu wowote watasimama katika kikao ambacho hawamtaji Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, isipokuwa watanyanyuka mithili ya mzoga wa punda, na wanakua na majuto

Hakuna watu wowote watasimama katika kikao ambacho hawamtaji Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, isipokuwa watanyanyuka mithili ya mzoga wa punda, na wanakua na majuto

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Hakuna watu wowote watasimama katika kikao ambacho hawamtaji Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, isipokuwa watanyanyuka mithili ya mzoga wa punda, na wanakua na majuto".

[Sahihi] [Imepokelewa na Abuu Daud]

الشرح

Maana ya hadithi: Nikuwa watakao kaa katika kikao chochote ambacho hawakumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake mfano wa hali yao ni kama yule unayekaa katika meza ya ugeni wake mzoga wa punda, ambao ni mzoga unaonuka zaidi na mchafu zaidi, na ananyanyuka katika kikao hicho kama anavyonyanyuka aliyeko katika mzoga huu, na huu ni mfano mdogo wa mtu anapofanya uzembe katika kumtaja Mwenyezi Mungu, basi watajuta majuto makubwa mno kwa yale waliyoyafanyia uzembe katika muda wao na wakaupoteza katika mambo yasiyokuwa na faida ndani yake. Hivyo ni wajibu kwa waislamu: wachunge sana vikao vyao kuwa ni vikao vya mambo ya utiifu na ibada na wavikimbie vikao vya mambo ya kipuuzi kama wanavyokimbia harufu mbaya na uchafu, kwani hakika mwanadamu ataulizwa juu ya muda wake, na atahesabiwa juu yake, ikiwa aliutumia kwa kheri basi itakuwa kheri, na ikiwa aliutumia kwa shari basi itakuwa ni shari.

التصنيفات

Fadhila za Adh-kaar.