Atakayesema: (Laa ilaaha illa llahu, wah-dahu laa sharika lahu, Lahul mulku, Walahul hamdu, Wahuwa alaa kulli shaini Qadiir) kwa siku mara mia moja

Atakayesema: (Laa ilaaha illa llahu, wah-dahu laa sharika lahu, Lahul mulku, Walahul hamdu, Wahuwa alaa kulli shaini Qadiir) kwa siku mara mia moja

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayesema: (Laa ilaaha illa llahu, wah-dahu laa sharika lahu, Lahul mulku, Walahul hamdu, Wahuwa alaa kulli shaini Qadiir) kwa siku mara mia moja, inakuwa kwakwe ni sawa na kuacha huru watu kumi, na anaandikiwa mema mia moja, na anafutiwa makosa mia moja, na inakuwa kwake ni kinga kutokana na Shetani kwa siku yake nzima mpaka afike jioni, na hatokuja yeyote na jambo bora zaidi kuliko atakalokuja nalo, isipokuwa yeyote atakayefanya zaidi ya alivyofanya yeye".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema: "Hapana Mola" na hakuna muabudiwa wa haki "isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika" katika uungu wake na ulezi wake na majina yake na sifa zake, "Ufalme ni wake" na maamuzi na mipangilio yote, "naye juu ya kila kitu ni muweza" pasina wa kumzuia wala wa kumkinga, na asiyoyataka hayawezi kuwa. Atakayesema dhikiri hii kwa siku mara mia moja, ataandikiwa ujira kutoka kwa Mwenyezi Mungu sawa na aliyeacha huru watumwa kumi, na ataandikiwa kwa maneno hayo mema mia moja na daraja Peponi, na yatafutwa kwake makosa mia moja, na yatakuwa ni kinga na kizuizi na ngome dhidi ya Shetani na upotovu wake na usaliti wake katika siku yake hiyo mpaka iingie jioni kwa kuzama jua, na hatoleta yeyote siku ya Kiyama kitu bora kuliko alichokuja nacho, isipokuwa mtu aliyefanya zaidi ya hivyo na akazidisha zaidi ya hapo.

فوائد الحديث

Ubora wa neno la Tauhidi na ukubwa wa malipo yake.

Upana wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya waja wake, kiasi ambacho kawawekea dhikiri nyepesi kwa kila mmoja, na akaipangia thawabu nyingi.

Ikiwa atasema dhikiri hii (Tahalil) zaidi ya mara mia moja katika siku, basi atapata malipo yaliyotajwa katika hadithi ya mia moja, na atakuwa na thawabu nyingine za ziada, na hii si katika mipaka iliyozuiliwa kuivuka, na kupitiliza idadi yake, na kwamba kuzidisha kwake hakuna fadhila au kunaibatilisha.

Amesema Nawawi: Dhahiri ya ujumla wa hadithi hii nikuwa anayapata malipo haya yaliyotajwa katika hadithi ni yule atakayesema tahlil hii (dhikiri) mara mia moja katika siku yake, sawa sawa awe aliyasema kwa mfululizo au tofauti tofauti katika vikao tofauti, au baadhi yake mwanzo wa mchana na mengine mwisho wake, lakini kilicho bora ayalete mfululizo mwanzo wa mchana, ili iwe ni kinga kwake katika mchana wake wote.

التصنيفات

Fadhila za Adh-kaar., Faida za Kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.