Ulimi wako usiache kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu

Ulimi wako usiache kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu

Kutoka kwa Abdallah bin Busri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika sheria za Uislamu zimekuwa nyingi kwangu, hebu nieleze kitu ambacho nitashikamana nacho, akasema: "Ulimi wako usiache kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu".

[Sahihi]

الشرح

Mtu mmoja alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ibada za sunna zimekuwa nyingi kwake mpaka zikamshinda kwa sababu ya udhaifu wake, kisha akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali nyepesi itakayompa thawabu nyingi atakayoshikamana nayo na adumu nayo. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuelekeza kuwa ulimi wake uwe mbichi utikisike kwa kudumu kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kila wakati na kila hali; kama kumsabihi na kumhimidi na kumtaka msamaha na kumuomba na mfano wake.

فوائد الحديث

Fadhila za kudumu na kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Miongoni mwa fadhila za Mwenyezi Mungu ni kufanya sababu za kupata malipo kuwa nyepesi.

Watu kuzidiana katika mafungu yao katika milango ya wema na kheri.

Kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi kwa ulimi, kwa kumsabihi na kumhimidi, na kukiri kuwa hapana mola muabudiwa wa haki ila yeye, na kumtukuza, na mengineyo pamoja na moyo kwenda sambamba na ulimi, hili linakaa nafasi ya ibada nyingi za sunna.

Kuchunga kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya muulizaji kwa kumjibu kila linalomfaa.

التصنيفات

Fadhila za Adh-kaar.