Atakayesema: Sub-haanallahi wabihamdihi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake) kwa siku mara mia moja (100), yatafutwa madhambi yake hata kama yatakuwa na wingi mfano wa povu la Bahari

Atakayesema: Sub-haanallahi wabihamdihi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake) kwa siku mara mia moja (100), yatafutwa madhambi yake hata kama yatakuwa na wingi mfano wa povu la Bahari

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayesema: Sub-haanallahi wabihamdihi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake) kwa siku mara mia moja (100), yatafutwa madhambi yake hata kama yatakuwa na wingi mfano wa povu la Bahari".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayesema kwa siku mara mia moja (100): "Sub-haanallaahi Wabihamdihi"; Yatafutwa makosa yake na yatasamehewa, hata kama yatakuwa mengi mfano wa taka nyeupe (povu) zinazoelea Baharini wakati mawimbi yanapotembea na yanapopiga.

فوائد الحديث

Malipo haya anayapata atakayelisema neno hilo ndani ya siku nzima mfululizo au kwa nyakati tofauti tofauti.

Tasbihi: Ni kumtakasa Allah kutokana na mapungufu, na kumhimidi: Ni kumsifu kwa ukamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza.

Makusudio katika hadithi hii ni kufutwa madhambi madogo madogo, ama madhambi makubwa haya ni lazima yafanyiwe toba.

التصنيفات

Fadhila za Adh-kaar.