Ama mimi sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu, lakini Jibril alinijia na kuniambia kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifaharisha kupitia nyinyi, huko kwa Malaika.!

Ama mimi sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu, lakini Jibril alinijia na kuniambia kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifaharisha kupitia nyinyi, huko kwa Malaika.!

Kutoka kwa Abuu Said Al-Khudri amesema: Muawia alitoka kwenda msikitini akakuta kundi, akasema: Nini kimewakalisha hapa? Wakasema: Tumekaa tukimkumbuka Mwenyezi Mungu. Akasema: Mnamuapa Mwenyezi Mungu kuwa hakuna lililowakalisha isipokuwa hilo? Wakasema: Wallahi hakuna lililotukalisha isipokuwa hilo. Akasema: Basi tambueni kuwa sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu kwa lolote, na hakuna aliyekuwa katika nafasi yangu kwakuwa na mazungumzo machache zaidi kuliko mimi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: Na hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, siku moja alitoka kwenda katika kundi la Maswahaba zake na kusema: “Mbona mmekaa pamoja?” Wakasema: Tumekaa tukimkumbuka Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa kuwa ametuongoza kwenye Uislamu, na kwa kutujaalia. Akasema: “Mnamuapa Mwenyezi Mungu kuwa hakuna lililokukalisheni isipokuwa hilo?" Wakasema: "Wallahi hatukukaa kwa lolote ila hilo.” Akasema: «Ama mimi sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu, lakini Jibril alinijia na kuniambia kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifaharisha kupitia nyinyi, huko kwa Malaika.!"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alitoka Muawia bin Abi Sufian, Mwenyezi Mungu awawie radhi, kwenda katika kundi moja msikitini na akawauliza wamekusanyika kwa jambo gani, Wakasema: Tunamtaja Mwenyezi Mungu, basi akawaapisha, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kwamba hawakutaka katika kikao chao na mkusanyiko wao isipokuwa ni kumtaja Mwenyezi Mungu, wakaapa kwa hilo, kisha akawaambia: Sikukuapisheni kwa tuhuma yoyote juu yenu au kuwa na shaka juu ya ukweli wenu, kisha akaeleza kuhusu hali yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba hakuna aliyekuwa karibu naye kuliko yeye. Kwa sababu Ummu Habiba alikuwa ni dada yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwa sababu alikuwa ni miongoni mwa waandishi wa wahyi, lakini ilikuwa ni nadra sana kusimulia hadithi, Basi akawaambia kuwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, siku moja alitoka nyumbani kwake na akawakuta wamekaa msikitini wakimdhukuru Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa yale aliyowaongoza katika Uislamu na kuwakirimia. Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, akawauliza na kuwaapisha sawa na alivyofanya Muawia kwa jamaa zake, Mwenyezi Mungu amuwie radhi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaambia kuhusu sababu ya kuwauliza kwake na kuapa kwao: kwamba Malaika Jibril, amani iwe juu yake, alimjia na kumwambia kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifakhirisha kupitia nyinyi kwa Malaika, na anawadhihirishia ubora wenu na anawaonyesha uzuri wa amali yenu, na anakusifieni mbele yao.

فوائد الحديث

Fadhila za Muawia, Mungu amuwie radhi, na pupa yake ya kumuiga Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake katika kufikisha elimu.

Inafaa kumwapiza mtu hata kama humtuhumu, bali kwa ajili tu kumzindua juu ya umuhimu wa kheri unayotaka kumueleza.

Fadhila za vikao vya kumtaja Mwenyezi Mungu, na vikao vya kielimu, nakuwa Mwenyezi Mungu huvipenda na hujifaharisha kwavyo mbele za Malaika.

التصنيفات

Ubora wa Elimu., Fadhila za Adh-kaar.