Mtakapo msikia muadhini basi semeni mfano wa yale anayo yasema, kisha mnitakie rehema

Mtakapo msikia muadhini basi semeni mfano wa yale anayo yasema, kisha mnitakie rehema

kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Yakwamba amemsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake anasema: "Mtakapo msikia muadhini basi semeni mfano wa yale anayo yasema, kisha mnitakie rehema, ni kwamba yule atakaye nitakia rehema mara moja Allah atamtakia rehema mara kumi, kisha niombeeni kwa Allah ukaribu, hakika ukaribu huo ni daraja ndani ya Pepo, halipati daraja hilo isipokuwa mja miongoni mwa waja wa Allah, na ninatarajia niwe mimi ndiye huyo mja huyo, na atakayeniombea mimi ukaribu ataupata uombezi".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ameelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mwenye kumsikia muadhini kwa ajili ya swala basi naye amfuatilize nyuma yake, aseme mfano wa kauli zake, isipokuwa haiala mbili (Hayya alas-swalaa, na hayya alal falaah), atasema baada yake: Laa haulaa walaa quwwata illa billaah, kisha atamtakia rehema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kumalizika kwa adhana, kwani atakayemtakiwa rehema mara moja, basi Mwenyezi Mungu atamtakia rehema kumi kwa sababu ya dua hiyo moja, na maana ya Mwenyezi Mungu kumtakia rehema mja wake: Ni kumsifu mja wake mbele ya Malaika. Kisha akaamrisha kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ukaribu -Rehema na amani ziwe juu yake-, nayo ni nafasi iliyoko peponi, na ni daraja ya juu zaidi kuliko zote, haimstahiki na wala haiwezekani nafasi hiyo ila kwa mja mmoja katika waja wote wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ninataraji mimi kuwa ndiye mja huyo, na alisema hivyo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa sababu ya kujinyenyekeza; kwa sababu nafasi hiyo ikiwa haistahiki ila kwa mtu mmoja, hawezi kuwa mmoja huyo zaidi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-; kwa sababu yeye ndiye mbora wa viume wote. Kisha akabainsha -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayemuombea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nafasi ya ukaribu basi ataupata utetezi wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

فوائد الحديث

Himizo la kumjibu muadhini.

Fadhila za kumtakia rehema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kumjibu muadhini.

Himizo la kumuombea ukaribu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kumtakia rehema.

Kumebainishwa maana ya ukaribu, na ukubwa wa nafasi yake, kiasi kwamba haumstahiki ila mja mmoja pekee.

Kumebainishwa ubora wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi ambacho kapendelewa nafasi hiyo ya juu.

Atakayemuomba Mwenyezi Mungu ukaribu kwa ajili ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- basi atastahiki kupata uombezi.

Kumebainishwa unyenyekevu wake -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi kwamba ameuomba umma wake umuombee dua ili apate nafasi hiyo, pamoja nakuwa nafasi hiyo itakuwa yake.

Upana wa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema yake, jema moja linalipwa kwa mema kumi mfano wake.

التصنيفات

Kuamini siku ya mwisho, Kuamini siku ya mwisho, Fadhila za Adh-kaar., Fadhila za Adh-kaar., Adhana na Iqama., Adhana na Iqama.