إعدادات العرض
1- Atakayeshuka mahala popote kisha akasema: -A'udhu bikalimaati llaahit taammaati min sharri maa khalaqa- (Najilinda kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia, kutokana na shari ya vile alivyoviumba), hakitomdhuru chochote mpaka aondoke mahala pake hapo
2- Hakika mimi ninajua neno ambalo laiti angelisema yangemuondokea yaliyompata, lau angelisema: Au'dhubillaahi minshaitwanir-rajiim, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani aliyelaaniwa, yangemuondokea yaliyompata
3- Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu