إعدادات العرض
Amepata hasara mtu nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema, na kapata hasara mtu ambaye itaingia Ramadhani mpaka ikatoweka kabla hajasamehewa, na kapata hasara mtu atakayewapata wazazi wake akiwa mtu mzima na wao wakiwa wazee na wakawa hawakumuingiza peponi
Amepata hasara mtu nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema, na kapata hasara mtu ambaye itaingia Ramadhani mpaka ikatoweka kabla hajasamehewa, na kapata hasara mtu atakayewapata wazazi wake akiwa mtu mzima na wao wakiwa wazee na wakawa hawakumuingiza peponi
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Amepata hasara mtu nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema, na kapata hasara mtu ambaye itaingia Ramadhani mpaka ikatoweka kabla hajasamehewa, na kapata hasara mtu atakayewapata wazazi wake akiwa mtu mzima na wao wakiwa wazee na wakawa hawakumuingiza peponi".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Português සිංහල অসমীয়া Tiếng Việt ગુજરાતીالشرح
Makundi matatu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliyaombea dua mbaya ya pua zao kugusa mchanga kwa udhalili na unyonge na hasara: Kundi la kwanza: Yule atakayetajwa mbele yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akawa hakumswalia, kwa kusema: Swalla llaahu a'laihi wasallam (Rehema na amani ziwe juu yake) na mfano wake. La pili: Ni yule atakayeupata mwezi wa Ramadhani kisha mwezi ukamalizika kabla hajasamehewa kwa uzembe wake wa kufanya mambo ya kheri. La tatu: Ni mtu atakayewapata wazazi wake wakiwa watu wazima, na hawakuwa sababu ya yeye kuingia peponi kwa sababu ya kuwaasi kwake na uzembe wake katika kutekeleza haki zao.فوائد الحديث
Amesema As-Sanadi: Kiuhalisia nikuwa kila mmoja katika hawa kapata jambo ambalo lau kama si uzembe basi angepata fungu kubwa katika kheri, wakati alipofanya uzembe mpaka likampita hilo basi atakuwa amefeli na kupata hasara.
Himizo la kumswalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kila linapotajwa jina lake.
Himizo la kujitahidi na kujikaza katika ibada ndani ya mwezi wa Ramadhani.
Himizo la kufanya juhudi kubwa katika kuwatendea wema wazazi wawili na kuwakirimu, hasa hasa wakati wa uzee.
التصنيفات
Adhkaar za mambo ya Dharura.