Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia

Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia

Kutoka kwa Hussein bin Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na An-Nasaaiy - Imepokelewa na Ahmad]

الشرح

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha kumtakia rehema wakati wa kusikia jina lake au wasifu wake, na akasema: Bahili kamili ni yule nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema; na hili ni kwa sababu ya mambo yafuatayo: La kwanza: Nikuwa ni ubahili kwa kitu ambacho mtu hapati hasara sawa iwe ndogo au kubwa, wala hatoi mali, na wala hatumii nguvu wala juhudi. La pili: Ni kuifanyia ubahili nafsi yake kwa sababu anainyima malipo ya kumtakia rehema Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake: kwa sababu anapojizuia kumtakia rehema atakuwa kafanya ubahili na kakataa kutimiza haki ya wajibu kwake kuitekeleza, kwa kutekeleza amri na akapata malipo. La tatu: Kumtakia rehema ndani yake kuna kutimiza haki za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, yeye ndiye aliyetufundisha, na yeye ndiye aliyetuelekeza, na yeye ndiye aliyetuita kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akaja na wahyi huu, na sheria hii, yeye ndiye sababu ya kuongoka kwetu baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, atakayeacha kumtakia rehema basi atakuwa kamfanyia ubahili Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake kwa kutompa haki ndogo kabisa miongoni mwa haki zake

فوائد الحديث

Kuacha kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni miongoni mwa alama za ubahili.

Kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni katika ibada bora anazojikurubisha kwazo mja katika nyakati zote, na inatiwa mkazo hasa wakati wa kutajwa kwake.

Amesema Imam Nwawi: Mtu akimsalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi akusanye kati ya kumsalia na kumtakia amani, na wala asiishie katika moja ya haya; Asiseme: "Rehema ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake" Pekee, wala: "Amani iwe juu uake" pekee.

Amesema Abul Aalia katika kauli yake: "Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii" Akasema: Sala ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake: Ni kumsifia, na sala ya Malaika na watu: Ni kumuombea dua.

Amesema Al-Hulaimi: Maana ya "Ewe Mwenyezi Mungu msalie Muhammad": Ewe Mwenyezi Mungu mtukuze katika dunia kwa kukuza kutajwa kwake, na kuidhihirisha dini yake, na kuibakiza sheria yake, na Akhera: Kwa kumfanya kuwa mtetezi wa umma wake, na kuyajaza malipo yake na thawabu zake, na kwa kuzionyesha wazi fadhila zake kwa wa mwanzo na wa mwisho kwa kumpa nafasi nzuri, na kwa kumtanguliza mbele kuliko wote waliokaribu nawe watakaoshuhudia Kiyama.

التصنيفات

Adhkaar za mambo ya Dharura.