Je, nisikujulisheni kitu bora zaidi kuliko hicho mlichoomba? Mtakapokwenda kulala basi msabihini Mwenyezi Mungu; yaani (Sub-haanallaah) mara thelathini na tatu, na mhimidini (Al-hamdulillaah) mara thelathini na tatu, na mtukuzeni (Allahu Akbar) mara thelathini na nne, kufanya hivyo ni bora zaidi…

Je, nisikujulisheni kitu bora zaidi kuliko hicho mlichoomba? Mtakapokwenda kulala basi msabihini Mwenyezi Mungu; yaani (Sub-haanallaah) mara thelathini na tatu, na mhimidini (Al-hamdulillaah) mara thelathini na tatu, na mtukuzeni (Allahu Akbar) mara thelathini na nne, kufanya hivyo ni bora zaidi kwenu kuliko mfanyakazi.”

Imepokelewa kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake-: ِAlikuja Fatma radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akimlalamikia juu ya jiwe la kusagia lililokuwa likichubua mikono yake, na zilimfikia taarifa kuwa Mtume amejiwa na mjakazi, lakini alikuwa hajakutana naye, akalieleza hilo kwa Aisha, alipokuja Aisha akamwambia, anasema Fatma: Akaja kwetu hali yakuwa tumekwisha panda kitandani, basi tukaamka tukasimama, akasema: "Haina haja ya kusimama kaeni tu mahala penu" Akaja akakaa kati yangu na Fatma, mpaka nikahisi ubaridi wa miguu yake tumboni kwangu, Mtume akasema: «Je, nisikujulisheni kitu bora zaidi kuliko hicho mlichoomba? Mtakapokwenda kulala basi msabihini Mwenyezi Mungu; yaani (Sub-haanallaah) mara thelathini na tatu, na mhimidini (Al-hamdulillaah) mara thelathini na tatu, na mtukuzeni (Allahu Akbar) mara thelathini na nne, kufanya hivyo ni bora zaidi kwenu kuliko mfanyakazi.”

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Fatima Mwenyezi Mungu amuwie radhi binti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilalamikia athari za mashine ya kusagia (Jiwe) aliyoipata mkononi mwake, hivyo alipokuja mtumwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuendea na kumuomba ampe mmoja kati ya watumwa hao, ili amsaidia kwa kazi za nyumbani, lakini hakumkuta Mtume nyumbani kwake, ila alimkuta Aisha Mwenyezi Mungu amuwie radhi, hivyo akamwambia kuhusu hilo, Alipofika rehema na amani ziwe juu yake Aisha akamueleza kuwa Fatma alikuja kwake kumuomba mfanyakazi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaja kwa Fatma na Ally Mwenyezi Mungu awawie radhi, ndani ya nyumba yao wakiwa wamelala kitandani wakijiandaa kwa usingizi, akakaa katikati yao mpaka Ally radhi za Allah ziwe juu yake akahisi ubaridi wa miguu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, juu ya tumbo lake, akasema: Hivi nisikufundisheni kilicho bora zaidi kuliko mlichoniomba, kuliko kukupeni mtumishi? Wakasema: Ndio, tufundishe, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Mtakapochukua nafasi zenu za kulala usiku, basi toeni takbira mara thelathini na nne, kwa kusema: Allahu Akbaru, Na toeni tasbihi mara thelathini na tatu, kwa kusema: Sub-haanallaah, Na himidini mara thelathini na tatu, kwa kusema: Al-hamdulillah; Dhikiri hii ni bora sana kwenu nyinyi kuliko kuwa na mtumishi.

فوائد الحديث

Inapendeza kudumu na dhikiri hi iliyobarikiwa, kama ilivyoripotiwa kuwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake hakuiacha amri hii ya Mtume iliyokusanya mambo mengi, mpaka katika usiku wa mapigano ya Swuffin.

Dhikiri hii haisemwi tu wakati wa kulala usiku, na maneno yake kwa mujibu wa Muslim yanatokana na riwaya ya Muadhi kutoka kwa Shu’ba: “Mkichukua vitanda vyenu wakati wa usiku.”

Muislamu akiisahau dhikri hii mwanzoni mwa usiku kisha akaikumbuka mwishoni mwa usiku, hakuna ubaya kuisema; Kwa sababu Ally Mwenyezi Mungu amuwie radhi, msimuliaji wa hadithi, anasema kwamba alisahau kuyasema katika usiku wa mapigano ya Swaffin mwanzoni mwa usiku, kisha akakumbuka na kuyasema kabla ya Alfajiri.

Amesema Al-Muhallab: Ndani ya Hadithi hii kunaonyesha kuwa mtu ailazimishe familia yake kufanya anayojilazimisha yeye, kama kutanguliza maisha ya Akhera kuliko Dunia hii ikiwa wana uwezo wa kufanya hivyo.

Amesema bin Hajar Al-Asqalani: Atakayedumu na dhikiri hii hatadhurika na wingi wa kazi, wala haitakuwa vigumu kwake hata akichoka.

Amesema Al-Aini: Suala la kuwa bora ni ima maana yake ni kuwa inahusiana na Akhera na mfanyakazi duniani, na Akhera ni bora zaidi na yenye kudumu, au ina maana kwamba kuhusiana na kile alichoomba atapata nguvu kwa sababu ya dhikiri hii ambayo itamuwezesha kufanya kazi zaidi kuliko uwezo wa mfanyakazi.

التصنيفات

Adhkaar za mambo ya Dharura.