Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguvu zangu, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia

Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguvu zangu, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia

Kutoka kwa Sahal bin Muadhi bin Anas kutoka kwa baba yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguvu zangu, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia".

[Ni nzuri]

الشرح

Anamhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kula chakula amshukuru Mwenyezi Mungu, kuwa mimi sina uwezo wa kuleta chakula wala kukila isipokuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na msaada wake, Kisha akatoa habari njema rehema na amani ziwe juu yake kwa yeyote atakayesema hivyo kuwa anastahili msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa dhambi zake ndogo ndogo zilizopita.

فوائد الحديث

Inapendeza kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu mwisho wa chakula.

Kuna ubainifu wa fadhila kubwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya waja wake, kwa kuwa amewaruzuku na kuwasahilishia riziki, na akalifanya hilo kuwa ni kafara ya kusamehewa madhambi.

Mambo ya waja yote yanatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na si kwa uwezo wao au nguvu zao, na mja ameamrishwa kufanya sababu.

التصنيفات

Adhkaar za mambo ya Dharura.