Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata

Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata

Kutoka kwa Salmaani bin Swurad -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa nimekaa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kukawa na watu wawili wakitukanana, mmoja wao uso wake ulikuwa mwekundu (kwa hasira) na ikavimba mishipa yake ya shingo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata" Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani", akasema: Hivi mimi ninawendawazimu?

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Walitukanana na kushutumiana watu wawili mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na ukawa mwekundu uso wa mmoja wao na ikavimba mishipa inayozunguka shingo yake. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi ninajua neno ambalo lau angelisema huyu aliyekasirika basi hasira zingemuondokea, lau angesema: Audhubillaahi mina sh-shaitwanir rajiim - Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa. Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jilinde kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani. Akasema: Hivi mimi ni mwendawazimu?! Alidhania kuwa hajilindi na Shetani isipokuwa mwenye wazimu.

فوائد الحديث

Pupa ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kutoa muongozo na kuelekeza, panapopatikana sababu zake.

Hasira hutokana na Shetani.

Amri ya kujilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa wakati wa hasira, amesema Mtukufu: "Na ikiwa uchochezi wa Shetani utakuchochea basi omba ulinzi wa Mwenyezi Mungu.." Mpaka mwisho wa Aya.

Tahadhari ya kutoa matusi na yenye kufanana na matusi kama kutoa laana, na chukizo la hayo; kwa sababu mambo haya hupelekea katika uharibifu baina ya watu.

Kunukuu nasaha kumpelekea ambaye hajazisikia ili anufaike nazo.

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake dhidi ya hasira; kwa sababu husukuma katika shari na ugomvi, na alikuwa rehema na amani ziwe juu yake hakasiriki isipokuwa yanapotendwa maharamisho ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hii ndio hasira nzuri.

Amesema Imam Nawawi katika kauli yake "Kwani unaniona mimi ninawazimu": Kauli hii inaonyesha kuwa msemaji alikuwa ni miongoni mwa wanafiki, au ni katika mabedui wakorofi.

التصنيفات

Tabia mbovu., Adhkaar za mambo ya Dharura.