إعدادات العرض
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua swala kwa takbira (Allaahu Akbaru) na kisomo kwa kuanza na Alhamdulillaahi Rabbil a'alamiin
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua swala kwa takbira (Allaahu Akbaru) na kisomo kwa kuanza na Alhamdulillaahi Rabbil a'alamiin
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua swala kwa takbira (Allaahu Akbaru) na kisomo kwa kuanza na Alhamdulillaahi Rabbil a'alamiin, na alikuwa anaporukuu hanyanyui wala hainamishi kichwa chake, lakini kati na kati, na alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu hasujudu mpaka alingane wima, na alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida hasujudu mpaka alingane sawa kwa kukaa, na alikuwa akisoma tahiyatu kila baada ya raka mbili, na alikuwa akiutandika mguu wake wa kushoto na kuusimamisha mguu wake wa kulia, na alikuwa akikataza mkao wa Shetani, na akikataza mtu kulaza mikono yake kama wanyama wakali, na alikuwa akihitimisha swala kwa salamu
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî دری Македонски Tiếng Việt Magyar ქართული ไทย অসমীয়া Nederlands ਪੰਜਾਬੀالشرح
Ameeleza Mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake sehemu ya swala ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba alikuwa akifungua swala yake kwa takbira ya kufungua swala, akisema: "Allaahu Akbaru", na akifungua kisomo kwa suratul Faatiha. "Alhamdulillaah Rabbil A''alamiin..." Na alikuwa anaporukuu baada ya kisimamo, hainui kichwa chake na wala hakishushi wakati wa rukuu, bali anakifanya kilingane sawa kikiwa kimenyooka, na akinyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu ananyooka wima kabla hajasujudu, na akinyanyua kichwa chake kutoka katika sijida ya kwanza, hasujudu sijida ya pili mpaka atuliazane akiwa amekaa. Na alikuwa akikaa baada ya kila rakaa mbili kwa ajili ya tahiyatu, na anasema: "Attahiyyatu lillaahi was swalawaatu wat twayyibaatu...", na alikuwa anapokaa baina ya sijida mbili au kwa ajili ya tahiyatu analaza mguu wake wa kushoto na kuukalia, na anasimamisha mguu wake wa kulia. Na anamkataza mwenye kuswali kukaa ndani ya swala yake kama mkao wa Shetani, nao ni kulaza miguu yake yote miwili katika Ardhi, na kukaa kwa pande zake mbili za nyuma, au kuambatanisha makalio yake na Ardhi na akasimamisha miguu yake na kuweka mikono yake katika Ardhi kama anavyoitandaza mbwa, au akalaza mwenye kuswali mikono yake kwa kuinyoosha katika sijida kama anavyoilaza mnyama mkali. Na alikuwa akihitimisha swala yake kwa salamu: "Assalaam alaikum warahmatullah" upande wa kulia mara moja na mara nyingine upande wa kushoto.فوائد الحديث
Kumebainishwa kiasi kidogo cha namna ya swala ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Uwajibu wa takbira ya kuhirimia swala, inayoharamisha kila kauli au kitendo kinachopingana na kauli za swala na vitendo vyake, na kwamba kinyume na namna hiyo hakuna namna nyingine inayofaa kuingia ndani ya swala.
Uwajibu wa kusoma Suratul Faatiha.
Uwajibu wa kurukuu, na jambo bora zaidi ndani yake ni kulingana sawa, bila kuinuka, wala kuinama.
Uwajibu wa kuinuka kutoka katika rukuu, na uwajibu wa kulingana sawa katika kisimamo baada yake.
Uwajibu wa kusujudu, na uwajibu wa kunyanyuka kutoka katika kusujudu, na kulingana sawa wakati wa kukaa baada yake.
Sheria ya kulaza mguu wa kushoto kwa mwenye kuswali na kusimamisha mguu wa kulia katika kukaa ndani ya swala, ama katika tahiyatu ya mwisho katika swala ambayo ina tahiyatu mbili kama Magharibi na Ishaa, sheria ni kukalia kalio moja (Tawaruku), na zimekuja hadithi zingine kuhusu hilo.
Katazo la kujifananisha na Shetani katika kukaa kwake, na hiyo ni mtu kukaa juu ya makalio yake na kulaza miguu yake juu ya Ardhi, au akaisimamisha na akakaa kati kati yake ikiwa katika Ardhi.
Katazo la kujifananisha na wanyama washambuliao katika kutandaza mikono yake, nayo ni kutandaza mikono yake mwenye kuswali katika Ardhi, kwani hilo ni ishara ya uvivu na udhaifu.
Katazo la kujifananisha na Shetani na wanyama katika vitendo vyao.
Uwajibu wa kuhitimisha swala kwa salamu, nayo ni dua kwa wenye kuswali na waliohudhuria na wema wasiokuwepo kwa kuwaombea amani dhidi ya kila shari na mapungufu.
Uwajibu wa kutulizana ndani ya swala.
