Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisoma katika rakaa mbili za (sunna ya) Alfajiri {Qul yaa ayyuhal kaafiruun} na {Qul huwallaahu ahad}

Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisoma katika rakaa mbili za (sunna ya) Alfajiri {Qul yaa ayyuhal kaafiruun} na {Qul huwallaahu ahad}

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisoma katika rakaa mbili za (sunna ya) Alfajiri {Qul yaa ayyuhal kaafiruun} na {Qul huwallaahu ahad}.

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akipenda kusoma katika rakaa mbili za sunna ya Alfajiri baada ya suratul-Fatiha, katika rakaa ya kwanza (Qul-yaa ayyula-kaafiruun), na katika rakaa ya pili suratul (Qul-huwallaahu ahad).

فوائد الحديث

Kupendeza kusoma sura hizi mbili baada ya suratul Fatiha katika swala ya sunna ya Alfajiri.

Sura hizi mbili zinaitwa suratul-Ikhalswi (Utakasifu); kwa sbaabu katika suratul Kafirun kuna kujiweka mbali na yote wanayoyaabudu washirikina kinyume na Mwenyezi Mungu, nakuwa wao pia si waja wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ushirikina wao unaporomosha matendo yao, nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa, na ni kwa sababu katika suratul-Ikhlaswi kuna kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kutakasa matendo kwa ajili yake na kubainisha sifa zake.

التصنيفات

Sifa za Swala.