إعدادات العرض
Timizeni safu ya mbele, kisha inayofuata, na kama kuna mapungufu basi yawe katika safu ya mwisho
Timizeni safu ya mbele, kisha inayofuata, na kama kuna mapungufu basi yawe katika safu ya mwisho
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Timizeni safu ya mbele, kisha inayofuata, na kama kuna mapungufu basi yawe katika safu ya mwisho".
[Sahihi] [Imepokelewa na Abu Daud na Nasai]
الترجمة
العربية Português دری Македонски Magyar Tiếng Việt ქართული বাংলা Kurdî ไทย অসমীয়া Nederlands ਪੰਜਾਬੀ Indonesia Hausa ភាសាខ្មែរ English ગુજરાતી Tagalog Русский मराठी മലയാളംالشرح
Amewaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanaume wenye kuswali kwa pamoja kukamilisha safu ya kwanza, kisha kukamilisha safu inayofuata, na kuendelea, na yakipatikana mapungufu katika safu basi yawe mapungufu haya katika safu ya mwisho.فوائد الحديث
Kumebainishwa sunna katika kulinganisha sawa safu.
Kwa wenye kuswali basi wasiache mapungufu katika safu ya mbele, bali yawe mapungufu katika safu ya nyuma.
