Hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya ninayoipenda zaidi kuliko dunia nzima

Hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya ninayoipenda zaidi kuliko dunia nzima

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Ilipoteremka: "Hakika Sisi tumekufungulia wewe, ewe Mtume, ufunguzi ulio waziwazi, ili akusamehe Mwenyezi Mungu" mpaka katika kauli yake: "Ushindi mkubwa" [Fat-hi: 1-5] marejeo ya hili ni katika suluhu ya Hudaibia, na wao wakiwa wamejawa na huzuni na unyonge, na alichinja vichinjwa vyake hapo Hudaibia, akasema: "Hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya ninayoipenda zaidi kuliko dunia nzima".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ameeleza Anasi bin Maaliki radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba ilipoteremka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kauli yake Mtukufu: "Hakika sisi tumekufungulia ewe Muhammadi ufunguzi wa wazi wazi (1) Ili akusameheme Mwenyezi Mungu yaliyotangulia katika madhambi yako na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika njia iliyonyooka (2) Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu (3) Yeye ndiye aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi imani juu ya imani yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye ujuzi, mwenye hekima (4) Ili awaingize Waumini wanaume na Waumini wanawake katika Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo, na awafutie makosa yao. Na huko ndiko kufuzu kukubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (5) [Al-Fat-hi: 1-5]. Hili lilikuwa Wakati wa kurejea kwake kutoka Hudaibia, na wakati Maswahaba wakiwa wamegubikwa na huzuni na unyonge, wakiwa wamezuiliwa kutekeleza Umra, kwa sababu ya yale waliyokubaliana katika mkataba, na dhana yao ilikuwa; yote hayo hayana masilahi na Waislamu, na walichinja vichinjwa vyao hapo Hudaibia, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwa hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya inayopendeka zaidi kwangu kuliko dunia nzima, kisha akaisoma.

فوائد الحديث

Kumebainishwa ukubwa wa yale aliyomneemesha Mwenyezi Mungu Mtukufu Mtume wake Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake katika ushindi mkubwa katika suluhu ya Hudaibia; pale aliposema kumwambia: "Hakika sisi tumekufungulia ufunguzi wa wazi wazi". mpaka mwisho wa aya mbili.

Kumebainishwa yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu Mtukufu Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, walipotii amri yake na wakanyenyekea, kiasi ambacho aliteremsha kwao kauli yake Mtukufu: "Ili awaingize waumini wa kiume na waumini wa kike Pepo zinazopita chini yake mito" mpaka mwisho wa aya.

Kumebainishwa fadhila za Mwenyezi Mungu juu ya Nabii wake, na kwa waumini kwa kuwaahidi ufunguzi na ushindi.

Amesema Assa'di katika kuitafsiri kwake aya hii: "Hakika sisi tumekufungulia ewe Muhammadi ufunguzi wa wazi wazi" [Al-Fatha], Ushindi huu uliotajwa hapa ni Mkataba wa amani wa Hudaibia, pale washirikina walipomzuilia Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake – alipokuja kwa ajili ya kufanya Umra, katika kisa kirefu, ambacho mwisho wake ulikuwa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - alifanya nao suluhu juu ya kumaliza vita kati yake na wao kwa muda wa miaka kumi, na kwamba atafanya Umra katika mwaka uliofuata, na kwamba anayetaka kuingia katika mkataba wa kusaidiana na Makuraishi, ana ruhusa ya kufanya hivyo, na anayetaka kuingia katika mkataba wa kusaidiana na Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake, basi anaweza kufanya hivyo. Na sababu ya hilo kwamba pindi watu walipopata amani kutokana na wao kwa wao, eneo la kulingania kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu likapanuka, na akawa kila Muumini katika sehemu yoyote iliyopo katika nchi hizo anaweza kufanya hivyo, na likamwezesha mwenye uchu wa kuujua ukweli wa Uislamu kuujua. Kwa hivyo watu wakaingia katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi wakati wa kipindi hicho. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akauita (mkataba huo) ushindi, na akauelezea kwamba ni ushindi ulio wazi. Kwa sababu makusudio ya kuziteka nchi za washirikina ni kuimarisha dini ya Mwenyezi Mungu na kuwapa ushindi Waislamu, na hili lilitokea kwa ushindi huo.

التصنيفات

Tafsiri ya Qur'an., Fadhila za Qur'an.