إعدادات العرض
1- Kilipomfikia Abuu Twalib kifo, Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alimuendea akamkuta Abdullahi bin Abii Umaiyya na Abuu Jahli wakiwa wake, Akasema kumwambia mgonjwa: Ewe baba mdogo, Sema Laa ilaaha illa llaah -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu-, neno ambalo nitakutetea kwalo kwa Mwenyezi Mungu.
2- Hakita simama Kiyama mpaka jua lichomoze kutoka upande wa Magharibi, na likichomoza na wakaliona watu wote wataamini
3- Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe
4- Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni wakweli wala ni waongo, na semeni hivi {Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yote yaliyoteremshwa kwetu sisi}
5- Mayahudi wameghadhibikiwa, na Wakristo ni wapotofu
6- Ikiwa utawaona wenye kufuata Aya zenye kutatiza basi hao ndiyo ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika aya
7- Akasema: "Watahesabiwa kwa hiyana waliyokufanyia na kukuasi na kukudanganya, na itahesabiwa adhabu yako uliyowapa
8- Hakika haya unayoyasema na kuwalingania watu ni mambo mazuri, ikiwa utatwambia juu ya haya tuliyoyafanya kama yana kafara
9- Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba
10- Kisha hakika bila shaka mtakuja kuulizwa kuhusu neema