Hakita simama Kiyama mpaka jua lichomoze kutoka upande wa Magharibi, na likichomoza na wakaliona watu wote wataamini

Hakita simama Kiyama mpaka jua lichomoze kutoka upande wa Magharibi, na likichomoza na wakaliona watu wote wataamini

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Hakita simama Kiyama mpaka jua lichomoze kutoka upande wa Magharibi, na likichomoza na wakaliona watu wote wataamini, na wakati huo: ((Mtu haitamfaa imani yake ambaye alikuwa hakuamini kabla, au imani yake haikufanya mambo ya kheri:158)) na kwa hakika kitasimama Kiyama na hali yakuwa watu wawili wametandaza nguo zao kwa ajili ya kuuza na kununua na wala hatoweza kuzikunja kutokana na uharaka wa Kiyama, na kwa hakika kitasimama Kiyama ghafla, na kwa hakika ataondoka mtu na maziwa aliyoyachukua kwenye chuchu za mnyama na wala asiwahi kuyanywa, na kitasimama Kiyama wakati anatengeneza josho la kunyweshea na wala asiwahi kunywesheleza, na kwa hakika kitasimama Kiyama na mmmoja wenu atainua tonge kupeleka mdomoni na wala asiweze kula."

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa miongoni mwa alama kubwa za Kiyama, ni kuchomoza jua kutoka upande wa Magharibi badala ya upande wa Mashariki, na watu wakiliona wataamini wote, Na wakati huo haitomfaa kafiri imani yake, wala hayatomfaa matendo mema wala kutubia. Kisha akatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Kiyama kitatokea ghafla; Kitatokea na watu watakuwa kwenye hali walizokuwa nazo na wapo kwenye mambo yao ya kimaisha; Na kitasimama Kiyama hali ya kuwa muuzaji na mnunuzi wamesambaza nguo zao lakini hawataweza kuuziana wala hawataweza kuzikunja. Na kitasimama Kiyama na hali ya kuwa mtu ameshika maziwa aliyoyakamua kutoka kwa Ngamia wake na wala hatoweza kuyanywa. Na kitasimama Kiyama na mtu atakuwa anatengeneza josho la kunyweshezea wanyama na kulisiriba na wala hatowahi kunywesheleza humo. Na kitasimama Kiyama na mtu atakuwa kainua tonge lake ili kulipeleka kinywani mwake ili ale na wala hatoweza kulila tonge hilo.

فوائد الحديث

Uislamu na toba hukubalika kabla jua halijatoka upande wa Magharibi.

Kuhimizwa kujiandaa kwa ajili ya Kiyama kwa kuwa na imani na kutenda yaliyo mema; Kwa sababu Kiyama kitakuja ghafla.

التصنيفات

Maisha ya Barzakhi(Baada ya kufa), Tafsiri za Aya