Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe

Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe

Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe,kisha muitaji ataita; Enyi watu wa peponi, basi watainua vichwa vyao na kuangalia, basi mwenye kuita atasema: Je mnamjua huyu? Nao watajibu: Ndiyo hayo ni Mauti, na wote kwa hakika wameyaona, kisha mwenye kuita atawaita: Enyi watu wa Motoni, basi watainua shingo zao na kuangalia, basi atawaambia na je mnamjua huyu basi watamjibu ndiyo haya ni Mauti, na wote kwa kakika wameyaona, hivyo basi yatachinjwa kisha atasema: Enyi watu wa Peponi,kaeni humo milele na hakuna kufa, na nyie watu wa motoni kaeni humo milele na hakuna kufa, kisha akasoma: "Na uwaonye siku ya majuto wakati hukumu ya kuingia peponi na motoni itakapotolewa Nao wapo kwenye kughafilika na wala hawaamini" (Surat Maryam:39)

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mauti yataletwa siku ya Kiyama, kwa mfano wa dume la kondoo lilochanganya rangi nyeupe na nyeusi, Basi ataita mwenye kuita: Enyi watu wa peponi! Basi watainua shingo zao na watainua vichwa vyao na wataangalia, Basi atawaambia: Je mnamjua huyu? Basi watasema: Ndiyo haya ni mauti, na wote kwa hakika wameyaona na kuyajua, Kisha muitaji ataita: Enyi watu wa Motoni, na watainua shingo zao na vichwa vyao na wataangalia, Basi atasema: Je mnamjua huyu? Hivyo watamjibu: Ndiyo, haya ni mauti, na wote wameyaona; Basi atachinjwa, kisha atasema mwenye kuita: Enyi watu wa peponi bakieni humo milele na hakuna kufa, na enyi watu wa Motoni bakieni humo milele na wala hakuna kufa, Na kumefanywa hivyo ili iwe ni ziada ya neema kwa waumini, na iwe ni adhabu yenye kuumiza kwa makafiri. Kisha akasoma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Na uwaonye siku ya majuto wakati hukumu ya kuingia peponi na motoni itakapotolewa, nao wapo kwenye kughafilika na wala hawaamini" Hivyo basi siku ya Kiyama watatenganishwa watu wa Peponi na watu wa Motoni, na wataingia wote kule walipopangiwa na kukaa humo milele, Basi atajuta mkosaji atapata mshituko na kujuta kwa nini hakufanya mema, na mwenye matendo machache pia kwa nini hakuzidisha mambo ya heri.

فوائد الحديث

Mafikio ya mwanadamu huko Akhera ni kukaa milele Peponi au Motoni,

Kunatolewa tahadhari kubwa kutokana na mshituko utakao kuwa siku ya Kiyama, na kuwa siku hiyo ni siku ya mfadhaiko na majuto.

Kumewekwa wazi kuhusu furaha ya kudumu kwa watu wa Peponi, na huzuni ya kudumu kwa watu wa Motoni,

التصنيفات

Kuamini siku ya mwisho, Sifa za pepo na moto., Tafsiri za Aya