إعدادات العرض
bali semeni: Tumesikia na tumetii tunataraji msamaha toka kwako ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako
bali semeni: Tumesikia na tumetii tunataraji msamaha toka kwako ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Ilipoteremka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ni wa Mwenyezi Mungu ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, na chochote mnachokidhihirisha, kati ya viliomo ndani ya nafsi zenu au mnachokificha, Mwenyezi Mungu anakijua, na atawahesabu nacho. Atamsamehe anayemtaka na atampatiliza anayemtaka. Na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu" [Al-Baqara: 284], anasema: Likawa gumu sana hilo kwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha wakashuka chini kwa kupiga magoti, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu tumepewa jukumu la matendo tunayoyaweza, kama Swala, Swaumu, na Jihadi, na Sadaka, na imeteremka juu yako aya hii wala hatuiwezi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Je hivi mnataka kusema kama walivyosema watu wa vitabu viwili kabla yenu, tumesikia na tumeasi? bali semeni: Tumesikia na tumetii tunataraji msamaha toka kwako ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako", wakasema: Tumesikia na tumetii tunataraji msamaha toka kwako ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako, walipoisoma kauli hiyo, zikadhalilika ndimi zao, akateremsha Mwenyezi Mungu punde tu baada ya hapo: "Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na Waislamu, (pia wameamini hivyo) wote wamemwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake, na Mitume wake hatutofautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na husema tumesikia na tumetii, tunakuomba msamaha Mola wetu na marejeo ni kwako" [Baqara: 285] walipofanya hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akaifuta, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mwenyezi Mungu hailazimishi nafsi yoyote isipokuwa yaliyo sawa na uweza wake. (Faida ya) yale iliyochuma (nafsi hiyo) ni yake na hasara ya yale iliyochuma ni juu yake. (Husema); Mola wetu usitutese kama tukisahau au tukikosa" [Al-Baqara: 286] Akasema: Ndiyo "Mola wetu na usitubebeshe mzigo kama uliowabebesha wale waliokuwa kabla yetu" Akasema: Ndiyo "Mola wetu usitutwike tusiyoyaweza" [Baqara: 286] Akasema: Ndiyo "na utusamehe na utufutie na uturehemu, Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tusaidie juu ya watu makafiri." [Baqara: 286] Akasema: Ndiyo.
الترجمة
العربية Português دری Македонски Tiếng Việt Magyar ქართული Bahasa Indonesia বাংলা Kurdî ไทย অসমীয়া Nederlands Hausa ਪੰਜਾਬੀالشرح
Alipoteremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake kauli yake: "Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyoko mbinguni na Ardhini" Kwa kuviumba na kuvimiliki, na maamuzi na kuvipangilia, "Na ikiwa mtadhihirisha" na mkaonyesha wazi na mkatangaza "yaliko ndani ya nafsi zenu" na vifua vyenu "au mkayaficha" mkayasitiri na kuyaficha ndani ya nyoyo zenu "atakuhesabuni Mwenyezi Mungu" siku Kiyama. "basi anamsamehe amtakaye" kwa fadhila zake na rehema zake, "na anamuadhibu amtakaye" kwa uadilifu wake, "na Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni muweza" hakimshindi chochote. Maswahaba walipolisikia hilo liliwapa uzito sana; kwa sababu ndani yake kuna kuadhibiwa mpaka kwa yale yaliyoko moyoni, miongoni mwa fikira. Wakamjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha wakashuka chini kwa kupiga magoti, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumepewa majukumu kabla ya hili miongoni mwa amali za mwili yale tuwezayo kuyafanya; mfano kama swala na swaumu na Jihadi na sadaka, lakini imeteremshwa kwako aya hii na wala hilo hatuliwezi. Akasema kuwaambia rehema na amani ziwe juu yake: Hivi mnataka kusema kama walivyosema Mayahudi na Wakristo: "Tumesikia na tumeasi"? bali semeni: "Tumesikia na tumetii, tunataraji msamaha kutoka kwako Mola wetu, na marejeo ni kwako", Maswahaba kuitika amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wakasema: Tumesikia na tumetii, tunataraji msamaha kutoka kwako Mola wetu, na marejeo ni kwako. Walipolizungumza hilo Waislamu kwa ndimi zao, na nyoyo zao zikatii; Mwenyezi Mungu akateremsha sifa njema kwa Mtume na Umma wake kwa kauli yake: "Ameamini Mtume yale yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake na waumini (pia wameamini hivyo)" na zikanyenyekea ndimi zao na nyoyo zao kwa amri ya Mwenyezi Mungu. "Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake, hatutofautishi yeyote katika Mitume wake". Bali tunawaamini wote "na wakasema tumesikia" kauli yako "na tumetii" amri yako, na tunaomba "maghufira yako Mola wetu" na msamaha wako, "na marejeo ni kwao" na mafikio siku itakaposimama hesabu, walipofanya hivyo, na wakasema walichoamrishwa kusema kama kudhihirisha usikivu na utiifu kwa amri za Mwenyezi Mungu; akaupunguzia Mwenyezi Mungu Umma huu na akaifuta aya hiyo, kwa kauli yake: "Hailazimishi Mwenyezi Mungu Nafsi ila kwa kadiri ya wasaa wake" na uwezo wake na nguvu zake na juhudi zake, "ina" thawabu "za yale iliyoyachuma" na kuyafanya miongoni mwa kheri, "na inabeba" adhabu "za yale iliyoyachuma" kama mzigo wa dhambi, na hamuadhibu Mwenyezi Mungu kwa dhambi la mtu mwingine, wala kwa yale yaliyotiwa wasi wasi na nafsi yake. "Mola wetu, usituadhibu" na ukatutesa "ikiwa tutasahau" tukawa hatukukumbuka, "au tukakosea" tukaiacha haki si kwa makusudi, Mwenyezi Mungu akawajibu kwa hilo akasema: Ndiyo, nimefanya hivyo. "Mola wetu Mlezi usitubebeshe mazito" na mashaka na magumu "kama ulivyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu" katika wana wa Waisraeli na wengineo, Mwenyezi Mungu akapokea na akasema: Ndiyo, nimefanya hivyo. "Mola wetu Mlezi na wala usitubebeshe tusiyoyaweza" miongoni mwa majukumu na mabalaa na mambo ambayo hatuwezi kuyabeba, akasema Mwenyezi Mungu: Ndiyo nimefanya hivyo, "na utusamehe" madhambi yetu na utufutie, "na utughufirie" madhambi yetu na uyasitiri, "na uturehemu" kwa rehema zako pana, "wewe ndiye Mole wetu" na bwana yetu; "tunusuru" kwa kusimamisha hoja na ushindi "kwa watu makafiri" katika kupigana nao na kupambana nao, Mwenyezi Mungu akapokea, akasema kuwaambia: Naam, nimefanya hivyo.فوائد الحديث
Kumebainishwa huruma ya Mwenyezi Mungu kwa Umma huu kwa sababu ya Nabii wake rehema na amani ziwe juu yake, aliyesema Mwenyezi Mungu katika kutukuza jambo lake: "Na hatukukutuma isipokuwa uwe ni huruma kwa walimwengu: [Al-Anbiyaa: 107].
Kuthibitika kufutwa kwa aya ndani ya Qur'ani tukufu, na kwamba ndani ya Qur'ani ziko aya zinazosomwa lakini hukumu yake ilifutwa haifanyiwi kazi.
Ubora wa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na utiifu wao na kujisalimisha kwao katika amri za Mwenyezi Mungu, na kutekeleza kwao amri ya Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake.
Hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa na hofu kubwa juu ya Umma wake usijekupita njia za Umma zilizotangulia kwa kuyakataa yale waliyopewa miongoni mwa amri za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Uwajibu wa kujisalimisha katika amri za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na tahadhari ya kuleta upinzani katika amri zake, na kwamba kitendo hiki kuna kujifananisha na watu wa kitabu.
Kumebainishwa ubora wa Umma huu juu ya Umma zilizotangulia, kiasi ambacho wao walisema kuwaambia Manabii wao: Tumesikia na tumeasi, na Umma huu ulisema: Tumesikia na tumetii.
Ubora wa Umma katika kuondolewa uzito juu yake na kujibiwa kwa dua ya kutoadhibiwa kwa kusahau au kukosea, na kuondolea ugumu juu yake uliokuwa kwa wale waliokuwa kabla yao, na kutobebeshwa kwake yale usiyoyaweza.
Mwenyezi Mungu Mtukufu hatubebeshi tusiyoyaweza, na wala hatulazimishi ila kwa kadiri ya uwezo wetu, na kwamba wasi wasi wote unaozunguka ndani ya vifua ikiwa hatutouendekeza, na hatukutulizana kwake, na hatukuufanyia kazi, basi huo haudhuru.
Dua hii ametueleza Mwenyezi Mungu Mtukufu kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na waumini, na akaiweka ndani ya kitabu chake; ili iwe ni dua kwa wale watakaokuja baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, basi ni katika dua ambazo inapaswa kuzihifadhi, na kuziomba kwa wingi.
