Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba

Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba

Na kutoka kwa Ibn Omari Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake: Ya kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwahutubia watu siku ya ufunguzi wa mji wa Makka, akasema: "Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba , basi watu wako aina mbili: Mwema mchamungu mtukufu kwa Mwenyezi Mungu, na muovu mbaya dhalili kwa Mwenyezi Mungu, na watu wote ni wana wa Adam, na amemuumba Mwenyezi Mungu Adam kutokana na udongo. Amesema Mwenyezi Mungu: "Enyi watu hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanaume na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila tofauti tofauti, ili mfahamiane, hakika mbora wenu kwa Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na ana habari (za mambo yote)" [Al Hujuraat: 13].

[Sahihi]

الشرح

Aliwahutubia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- watu siku ya ufunguzi wa mji wa Makka akasema: Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu amenyanyua na akaondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga na kujiona, na kujifaharisha kwa baba zenu (nasaba), bali watu wako aina mbili: Ni ima muumini mwema, mchamungu, mtiifu, mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, huyu ni mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu, hata kama hana cheo au nasaba nzuri mbele za watu. Na ima kafiri muovu, na huyu ni dhalili kwa Mwenyezi Mungu, na wala hana thamani yoyote, hata kama ana ukoo mzuri na cheo na mamlaka. Na watu wote ni watoto wa Adam, na Mwenyezi Mungu kamuumba Adam kutokana na udongo, haifai kwa kiumbe ambaye asili yake ni udongo kuwa na kiburi na kujiona yeye ni bora, na hili linasadikishwa na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi watu! hakika sisi tumekuumbeni nyinyi kutokana na mwanaume na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila ili mpate kujuana, hakika mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na ana habari (ya myafanyayo) [Alhujrat:13].

فوائد الحديث

Katazo la kujifaharisha kwa ukoo na vyeo.

التصنيفات

Ubora wa uislamu na uzuri wake., Kuenea kwa dini ya uislamu., Haki za Mwanadamu katika uislamu, Tafsiri za Aya