إعدادات العرض
1- Shikamaneni na hii Qur'ani, Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mkononi mwake, hiyo ni nyepesi sana kuponyoka kuliko ngamia kuponyoka kutoka kwenye kamba yake.
2- Mbora wenu ni yule aliyejifunza Qur'ani na akaifundisha
3- Msizifanye nyumba zenu kuwa makaburi, hakika shetani huikimbia nyumba
4- Atakayezisoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara katika wakati wa usiku zitamtosheleza
5- Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja na jema hilo kwa mema kumi mfano wake
6- Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Nimeigawa swala baina yangu na mja wangu nusu mbili, na mja wangu ana haki ya kupata alichooomba
7- Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa chenza harufu yake nzuri na ladha yake nzuri, na mfano wa muumini ambaye hasomi Qur'ani ni kama mfano wa tende: haina harufu na ladha yake ni tamu
8- Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma
9- Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi?" Akasema: Nikasema: {Allahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayyuum} Al-baqara: Basi akanipiga katika kifua changu, akasema: Nakuombea Mwenyezi Mungu elimu ikupe furaha ewe baba Mundhir
10- Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapolala kitandani kwake wakati wa kila usiku alikuwa akikusanya viganja vyake, kisha akivipuliza na kuvisomea : {Qul-huwallahu Ahad}, na {Qul-A uudhu birabbil falaq} na (Qul-Auudhu birabbi naas }