Shikamaneni vizuri na hii Qur'ani, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hutoroka kwa kasi mno kuliko hata Ngamia katika kamba yake

Shikamaneni vizuri na hii Qur'ani, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hutoroka kwa kasi mno kuliko hata Ngamia katika kamba yake

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary-Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Shikamaneni vizuri na hii Qur'ani, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hutoroka kwa kasi mno kuliko hata Ngamia katika kamba yake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kushikamana na Qur'ani na kudumu na kuisoma ili mtu asiisahau baada yakuwa kaihifadhi katika kifua chake, na akalisisitiza hilo kwa kiapo chake -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba Qur'ani hujitoa haraka mno na kuondoka kutoka vifuani kuliko hata Ngamia aliyefungwa, naye ni yule aliyekazwa kwa kamba kati kati ya muhundi, mtu akikaa karibu naye atamshika, na akimuacha ataondoka na atapotea.

فوائد الحديث

Aliyehifadhi Qur'ani akidumu katika kuisoma kila mara itabakia kuwa imehifadhiwa katika moyo wake, na asipofanya hivyo itaondoka na ataisahau.

Katika faida za kushikana na Qur'ani ni: Malipo na thawabu, na kunyanyuliwa daraja siku ya Kiyama.

التصنيفات

Ubora wa kuutilia umuhimu Qur'an.