إعدادات العرض
1- Shikamaneni na hii Qur'ani, Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mkononi mwake, hiyo ni nyepesi sana kuponyoka kuliko ngamia kuponyoka kutoka kwenye kamba yake.
2- Mbora wenu ni yule aliyejifunza Qur'ani na akaifundisha
3- Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja na jema hilo kwa mema kumi mfano wake
4- Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa chenza harufu yake nzuri na ladha yake nzuri, na mfano wa muumini ambaye hasomi Qur'ani ni kama mfano wa tende: haina harufu na ladha yake ni tamu
5- Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma