إعدادات العرض
Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa chenza harufu yake nzuri na ladha yake nzuri, na mfano wa muumini ambaye hasomi Qur'ani ni kama mfano wa tende: haina harufu na ladha yake ni tamu
Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa chenza harufu yake nzuri na ladha yake nzuri, na mfano wa muumini ambaye hasomi Qur'ani ni kama mfano wa tende: haina harufu na ladha yake ni tamu
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa chenza harufu yake nzuri na ladha yake nzuri, na mfano wa muumini ambaye hasomi Qur'ani ni kama mfano wa tende: haina harufu na ladha yake ni tamu, na mfano wa mnafiki mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa Ua la Raihana harufu yake nzuri lakini ladha yake chungu, na mfano wa mnafiki ambaye hasomi Qur'ani ni kama mfano wa tango pori, halina harufu na ladha yake chungu".
الترجمة
العربية Bosanski English فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी Español Kurdî Português සිංහල Svenska ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá ئۇيغۇرچە Tiếng Việt Hausa پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or Malagasy Čeština नेपाली Oromoo Română Nederlands Soomaali తెలుగు മലയാളം Српски ไทย Kinyarwanda ಕನ್ನಡ Lietuviųالشرح
Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake migawanyiko ya watu katika kuisoma Qur'ani na kunufaika nayo. Sehemu ya kwanza: Ni muumini anayesoma Qur'ani na ananufaika nayo, yeye ni mfano wa chenza, lina ladha nzuri na harufu nzuri na rangi nzuri, na manufaa yake ni mengi, kwani yeye huyafanyia kazi anayoyasoma, na kuwanufaisha waja wa Mwenyezi Mungu. Sehemu ya pili: Ni muumini asiyeisoma Qur'ani, yeye ni mfano wa tende, ladha yake tamu, lakini haina harufu, moyo wake umejawa na imani mfano wa tende ilivyojawa utamu katika ladha yake na juu yake, na kutosikika harufu yake ambayo watu huinusa; kwa kutosikika kisomo toka kwake ambacho watu watapata raha kwa kukisikiliza Sehemu ya tatu: Mnafiki anayesoma Qur'ani, yeye ni mfano wa Ua Raihana, lina harufu nzuri na ladha yake chungu, kwakuwa hakuurekebisha moyo wake kwa imani, na hakuifanyia kazi Qur'ani, na anaonekana mbele za watu kuwa ni muumini, harufu yake nzuri inafanana na kisomo chake, na ladha ya chungu inafanana na ukafiri wake. Sehemu ya nne: Mnafiki asiyeisoma Qur'ani, yeye ni mfano wa tango pori, kiasi kwamba halina harufu nzuri, na ladha yake ni chungu, kukosekana kwa harufu yake kumefanana na harufu yake; kwa kutoisoma, na uchungu wa ladha yake unafanana na uchungu wa ukafiri wake, ndani mwake kuko tupu hakuna imani, na nje yake hakuna manufaa, bali kuna madhara.فوائد الحديث
Kumebainishwa ubora wa mwenye kuibeba Qur'ani mwenye kuifanyia kazi.
Miongoni mwa njia za ufundishaji ni kupiga mifano; ili kusogeza karibu uelewa.
Inatakiwa muislamu awe na kiwango maalum cha fungu katika kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
التصنيفات
Ubora wa kuutilia umuhimu Qur'an.