Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema hilo hulipwa mara kumi mfano wake

Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema hilo hulipwa mara kumi mfano wake

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema hilo hulipwa mara kumi mfano wake, sisemi (Alif Laam Miim) ni herufi, lakini (Alif) ni herufi, na (Laam) ni herufi, na (Miim) ni herufi".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila muislamu anayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na huzidishiwa malipo hayo mpaka mara kumi mfano wake. Kisha akaliweka wazi hilo kwa kauli yake: (Sisemi "Alif Laam Miim" ni herufi, lakini Alif ni herufi, na Laam ni herufi, na Miim ni herufi): Inakuwa herufi zote tatu zina thawabu thelathini (30).

فوائد الحديث

Himizo la kukithirisha kusoma Qur'ani.

Msomaji kwa kila herufi anayoisoma kwa kila neno analolisema huzidishwa mara kumi mfano wake.

Upana wa rehema za Allah na ukarimu wake kiasi kwamba huzidishwa malipo kwa waja ikiwa ni fadhila na ukarimu toka kwake.

Ubora wa Qur'ani juu ya maneno mengine, na kisomo chake kutumika kama ibada; nakuwa hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

التصنيفات

Ubora wa kuutilia umuhimu Qur'an., Ubora wa Qur'an tukufu.