إعدادات العرض
Anayesoma Qur'ani kwa uhodari huwa pamoja na msafara wa Malaika watukufu, na anayesoma Qur'ani huku anasitasita na huku kwake bado ni ngumu huyo anamalipo mara mbili
Anayesoma Qur'ani kwa uhodari huwa pamoja na msafara wa Malaika watukufu, na anayesoma Qur'ani huku anasitasita na huku kwake bado ni ngumu huyo anamalipo mara mbili
Kutoka kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Anayesoma Qur'ani kwa uhodari huwa pamoja na msafara wa Malaika watukufu, na anayesoma Qur'ani huku anasitasita na huku kwake bado ni ngumu huyo anamalipo mara mbili".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Français සිංහල Hausa Kurdî Português Русский Tiếng Việt Nederlands অসমীয়া ગુજરાતી Magyar ქართული Românăالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba anayesoma Qur'ani, akiwa na hifdhi nzuri na mfanisi, na mahiri na hodari kwa kisomo chake, basi huyu ana thawabu Akhera kiasi cha daraja yake kuwa pamoja na Malaika wema na wakarimu, na kwamba anayesoma Qur'ani na huku akipata tabu ndani yake na anasitasita katika kisomo chake; kwa sababu ya udhaifu wa hifudhi yake, lakini pamoja na hivyo bado anashikamana nayo, na kwake bado ni ngumu na nzito basi ana malipo mara mbili; malipo ya kisomo na malipo ya tabu na kusitasita kwake katika kisomo.فوائد الحديث
Himizo la kuhifadhi Qur'ani na kuwa na ustadi, na kuisoma kwa wingi kwa ajili ya kupata malippo na thawabu, na kumebainishwa nafasi ya mwenye kufanya hivyo.
Amesema Kadhi: Na haina maana kuwa anayesitasita ana malipo makubwa zaidi kuliko mahiri, bali mahiri ndiye bora na ndiye mwenye malipo mengi; kwa sababu yuko pamoja na Malaika na anamalipo mengi, na hakutaja nafasi hii kwa mwingine, ni vipi ataungana naye ambaye hajakipa kipaumbele kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kukihifadhi na kuwa na umahiri na wingi wa kukisoma na kukielewa kwake ni kama kukipa kipaumbele mpaka akawa mahiri ndani yake.
Amesema bin Bazi: Anayesoma Qur'ani hali yakuwa ni mahiri, na anaisoma vizuri, na anaihifadhi vizuri yuko pamoja na Malaika wema watukufu, yaani: Ikiwa kama ataisoma kwa kauli na matendo, na si ilimradi kuisoma pekee, anaisoma vizuri, na anaifanyia kazi, yaani anaisimamia kwa lafudhi na maana.