إعدادات العرض
Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, hakika Shetani hukimbia kutoka katika nyumba inayosomwa suratul Baqara ndani yake
Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, hakika Shetani hukimbia kutoka katika nyumba inayosomwa suratul Baqara ndani yake
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, hakika Shetani hukimbia kutoka katika nyumba inayosomwa suratul Baqara ndani yake".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية Bosanski English فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी বাংলা Español Kurdî Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் සිංහල မြန်မာ ไทย Deutsch 日本語 پښتو Tiếng Việt অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands ئۇيغۇرچە Hausa دری Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy Română Kinyarwanda नेपाली Српски Soomaali Moore Українська Български Tagalog Wolof Azərbaycan ქართული тоҷикӣالشرح
Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuyatelekeza majumba kwa kutoka swali ndani yake, yakawa kama makaburi yasiyoswaliwa ndani yake. Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Shetani hukimbia nyumba ambayo husomwa suratul Baqara ndani yake.فوائد الحديث
Kumependekezwa kuzidisha ibada na swala za sunna ndani ya majumba.
Haifai kuswali makaburini; kwa sababu ni njia katika njia za shirki na kuwakweza wafu, isipokuwa swala ya jeneza.
Katazo la kuswali makaburini limethibiti kwa Masahaba, na kwa sababu hiyo amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nyumba kufanywa mfano wa makaburi hakuswaliwi ndani yake.
التصنيفات
Fadhila za Sura na Aya.