Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi?" Akasema: Nikasema: {Allahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayyuum} Al-baqara: Basi akanipiga katika kifua changu, akasema: Nakuombea Mwenyezi Mungu elimu ikupe furaha ewe baba Mundhir

Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi?" Akasema: Nikasema: {Allahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayyuum} Al-baqara: Basi akanipiga katika kifua changu, akasema: Nakuombea Mwenyezi Mungu elimu ikupe furaha ewe baba Mundhir

Imepokelewa kutoka kwa Ubaiyya bin Kaab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi kwako?" Akasema: Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wajuzi zaidi. Akasema: "Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi?" Akasema: Nikasema: {Allahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayyuum} Al-baqara: Basi akanipiga katika kifua changu, akasema: Nakuombea Mwenyezi Mungu elimu ikupe furaha ewe baba Mundhir."

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimuuliza Ubaiyya bin Kaab kuhusu aya tukufu zaidi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu, akasitasita katika kutoa jibu, kisha akasema: Aya hiyo ni Ayatul Kursiy {Allahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayyuum} basi- Rehema na amani ziwe juu yake- akamuunga mkono, na Mtume akapiga katika kifua chake ikiwa ni ishara ya kifua hicho kujaa elimu na hekima, na akamuombea awe na furaha kwa elimu hii na Allah amfanyie wepesi.

فوائد الحديث

Fadhila kubwa alizokuwa nazo Ubaiyya bin Kaab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-

Ayatul Kursiy ni Aya tukufu zaidi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo inapasa kuihifadhi na kuzingatia maana yake pamoja na kuifanyia kazi.

التصنيفات

Fadhila za Sura na Aya., Fadhila za Sura na Aya., Ubora wa Elimu., Ubora wa Elimu.